Akiongea na FC mmoja wa waratibu wa tamasha hilo Mary Birdi amesema kuwa ni tamasha ambalo linaleta mabadiliko makubwa katika tasnia ya filamu Swahiliwood, kwani watengeneza filamu kutoka sehemu mbalimbali watafika na kubadilisha mawazo na watengezaji wa filamu wa Tanzania, ni muhimu kila mdau akajipanga na kushiriki tamasha hili linalojenga.
“Ni tamasha ambalo linajenga tasnia ya filamu nchini hasa pale watu wetu wanavyopata workshop kwa ajili ya kazi wanazofanya, siku hizi teknorojia inakwenda kwa kasi ni vema kupata shortcourse mara kwa mara, lakini ni nafasi pia ya kutangaza Utalii wetu,”anasema Mary.
Tamasha la AAFF litazinduliwa tarehe 29.November.2013 Mount Meru Hotel Jijini Arusha wakati Semina sitaanza rasmi tarehe 25.
November. 2013 sambamba na maonyesho ya filamu katika sehemu zifutazo Alliance Francaise, Via Via, Mount Meru Hotel, Mango Tree, na New Arusha Hotel tamasha hili kiingilio ni bure kabisa, Siku 7 USIKOSE KUSHUHUDIA FILAMU KALI KUTOKA SEHEMU MBALIMBALI.
No comments:
Post a Comment