Mwanafunzi aliyekuwa akisubiri kufanya mtihani wa kidato cha nne unaotaraji kuanza kesho Bw Khamis Mkundo mkazi wa Mwangata C katika Manispaa ya Iringa akiwa amejinyonga usiku huu kuhofu mtihani wa kidato cha nne
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mwangata C Bw Sarehe Mgimwa akisoma ujumbe ulioachwa na marehemu huyu
Hii ndo Barua ilioachwa na marehemu huyo
Mwanafunzi aliyekuwa akisoma shule ya sekondari Sabasaba mjini Iringa akijiandaa kurudia kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne kupitia kituo cha Krelluu mjini Iringa Khamis Mkundo mkazi wa Mwangata C katika manispaa ya Iringa amejiua kwa kujinyonga kwa kamba kwa kile alichodai kuchoshwa na kufeli mara kwa mara mtihani wa kidato cha nne.
Katika barua yake ndefu aliyoiandika kijana huyo amesema kuwa amefanya hivyo si kwa kujipendea ila amechukizwa na hatua yake ya kufeli mara kwa mara hivyo kuamua kujiua ili kuepuka na aibu katika mtihani ujao ambao anaamini angefeli.
Kwani alisema hajapenda kuona anaendelea kufeli na kuwa yupo tayari kwa lolote kukwepa aibu ambayo ipo mbele yake.
Hata hivyo kufuatia mazungumzo hayo kijana huyo aliangana na ndugu zake akiwemo kaka yake anayeishi nae kwa kila mmoja kuondoka nyumbani hapo kabla ya kijana huyo kukutwa amejinyonga.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Sarehe Mgimwa amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kuonyesha ujumbe ambao kijana huyo ameuacha
4 comments:
Hilo ni kweli kabisa, it doesn't make sense at all, hii abuse of the dead person, u supposed to treat dead body with dignity. .badilikeni waandishi jamani..
Nakanusha kabisa wewe muandishi hapo juu... Huwezi kueleza habari bila picha na hao watoto wanaosoma blogs wanatakiwa waone ndio wajifunze. Nakuunga mkono DJ Luke na endelea kutupa picha na matukio hakuna mtu anasoma habari bila kuona picha... Na wewe hapo juu angalia blog zote duniani zinatoa habari na picha ... Ukiweka habari bila picha nanai ataangalia blog yako.?? Picha ina represent feelings ukisoma habari bila picha hutapata uhondo inatakiwa uone picha ndio habari uielewe vizuri wakati mwingine picha tu inatoa maelezo bila hata kusoma mlolongo mzima kama mimi sina muda wa kusoma na ninajua watu wengi hawana muda wa kusoma maelezo marefu ila kukiwa na picha tunajua kinachoendelea.. Endelea kutuwekea picha na maelezo tafadhali sana ...
Post a Comment