7. HUMPI MPAKA AKATOSHEKA
Kama bado unaamini ‘romansi’ ni mchakamchaka wa kupashana joto kabla ya tendo, basi unahitaji elimu mpya na ukishaelimika, utabadili mtazamo wako. Bila shaka utaongeza muda wako wa ‘kudili’ na eneo husika. Hutaona matokeo yako mazuri faragha kama hutazingatia kipengele hiki.
Ufafanuzi upo hivi, romansi ni sehemu ya tendo la faragha, yaani ni mapenzi yenyewe. Huwezi kutenganisha mambo hayo mawili. Wengi hudhani yapo tofauti, hivyo kupoteza umakini na utendaji unaofaa katika romansi ambayo kwa hakika huhitaji muda wa kutosha.
Wale ambao hutofautisha romansi na tendo la faragha, hushindwa kuwa makini na kujua nini hasa wakifanye ili kuhakikisha mwanamke anatosheka. Kurukia tendo maana ni sawa na kukatiza njia ya mkato, kwa hiyo mwenzi wako atabaki njiani tu.
Hapa nikufafanulie kwamba usijidanganye mwanamke anapofika kileleni na kushusha mzigo, ukakaa na kujisifu kwamba wewe ni kidume. Jiulize; je, ameridhika? Ametosheka? Maana ya kukutaka ujiulize hivyo ni kwa sababu kuna tofauti kubwa kati ya kushusha mzigo na kuridhika.
Mwanamke hutosheka endapo tu utaenda naye hatua kwa hatua, huku ukitumia muda wako kushughulika na kila kipengele. Usikimbilie hatua ya mbele na kuzisahau zile za awali, kila moja ina umuhimu wake.
Ni muhimu kama mwanaume utambue kwamba mwanamke huhesabu romansi kuwa mapenzi, wengine huridhika zaidi katika kipengele hicho kabla ya tendo ambalo hufuata ambalo kiuhalisia huwa lina maana zaidi kwa wanaume katika kufika mshindo.
Ni vigumu sana kwa mwanamke kufikia mshindo ikiwa hatapata jeramba la kutosha. Usikimbilie kusimika mkwaju ‘uani’, haraka zote za nini? Nenda taratibu, mapenzi huhitaji muda wa kutosha. Achana na mtazamo wa kale, nenda kisasa uone matunda yake.
Ni lazima uelewe kuwa zipo hasara ambazo utakutana nazo kutokana na tabia ya kukariri mwendo wa shoka moja mbuyu chini. Kwanza mwenzi wako atakuona hujui mambo na atakushusha thamani, vilevile hutamridhisha, kwa hiyo anaweza kupepesa macho pembeni kuangaza atakayemtosheleza.
Chukua mfano huu; huwezi kuchukua mchi na kuanza kutwanga kwenye kinu bila maandalizi. Lazima kinu kisafishwe, kama kinachotwangwa ni hasimu wa maji, basi ni sharti kinu kiachwe kikauke ndipo kinacholengwa kiweke panapohusika ndiyo kitwangwe.
Kama mfumo ni huo, sasa wewe utaratibu wa njia ya mkato umeupata wapi? Kama ulishafanya makosa huko nyuma ni wakati wako sasa kujisahihisha. Hakikisha unamtosheleza kila hatua ndipo uende naye kwenye kipengele cha mwisho ambacho kwa kawaida, wewe ndiye hufaidi zaidi.
Ukifanya hivyo, utafanikiwa kumfikisha kileleni. Hapo ndipo unaweza kumfanya atosheke. Ndivyo atakavyokuheshimu, vilevile utampa sababu ya kutokusaliti. Unaweza kupiga mbizi kwa muda mfupi lakini akawa ametosheka kwa sababu ulitumia muda wa kutosha wakati wa jeramba (romansi).
Itaendelea wiki ijayo.
GPL
1 comment:
Luka hii inabidi uirudie kwa wiki nzima maana wadogo zako wengi wanapoteza wake kwa kutojua kutwanga na kupepeta kitaalam
Post a Comment