ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 18, 2013

MTOTO ANAYEDAIWA KUFUFUKA ANENA

Ni hivi karibuni, Mji wa Geita na maeneo jirani ulikubwa na taharuki ya aina yake,pale mtoto Shabani Maulid (15) anaedaiwa kwamba alifariki dunia miaka miaka mitatu iliyopita, alipoonekana akiwa hai katika Kijiji cha 14 Kambarage, Mtaa wa Mbugani.

Maulidi alitoweka ghafla Januari 1, 2011. Wazazi wake wanasema siku hiyo aliondoka nyumbani asubuhi na kupeleka mbuzi malishoni, na kwamba siku hiyo hakurudi, jambo lililowatia mashaka wazazi wake hivyo kuamua kutoa taarifa polisi na kwa uongozi wa kijiji.PICHA|MAKTABA
Hali hiyo iliwalazimisha wazazi wake kushirikiana na Jeshi la Polisi kumpeleka Haospitali ya Wilaya ya Geita ili apatiwe matibabu, lakini ni kama hawakuona mtoto wao akipata nafuu hivyo waliondoka naye na kuamua kumpeleka Kigoma Kambako anapatiwa tiba za jadi.

Tukio hilo lilizua hofu kwa wakazi wa Mji wa Geita huku waliowengi wakitaka kujua mtoto huyo aliyekutwa amefariki dunia baada ya kupotea kwa siku nne mwaka 2011 na mwili wake kuzikwa, inakuwaje leo hii anaonekana akiwa hai?
Tukio hilo lililotokea Septemba mwaka huu linashuhudiwa na wazazi wa Shaban, ndugu zake, jamaa na hata majirani wa eneo hilo ambao pia wanahoji, je aliyezikwa wakati mwili wa mtoto huyo ulipookotwa ni nani na je mwili wake uko kaburini au la?

Maswali haya na mengine, yalikosa majibu kwani baada ya kuonekana kwake, Shaban hakuweza kuongea vizuri na alionekana kutofahamu kabisa Kiswahili, lugha ambayo kabla ya kutoweka kwake aliifahamu vyema. Wakati huu mtoto huyu anaongea Kiha, japo nayo kwa tabu.

“Niliamua nimpeleke kwa waganga wa jadi huku nyumbani Kigoma na sasa hali inaendelea vizuri kwani anaweza kuongea japo ni kwa muda mfupi kisha hunyamaza”, alisema baba mzazi wa mtoto huyo, Maulidi.

Shaban alikuwa wapi?
Shaban hivi sasa anaendelea vizuri na ‘tiba’ anayopata huko Kigoma na aliweza kuzungumza na gazeti hili kwa simu, huku akieleza kutoweka kwake, pia huko alikokuwa kwa miaka mitatu, huku akiweka bayana kwamba hivi sasa anawatambua vizuri

wazazi na ndugu zake.

Alisema anakumbuka Januari 1, 2011 aliondoka nyumbani kwao na kuelekea malishoni kuchunga mbuzi, na wakati akiwa machungani ghafla lilitokea kundi la watu ambalo lilimzunguka.

Shabani anasema katika kundi hilo alikuwamo mwanamke ambaye hakumtaja kwa maelezo kwamba anashindwa kutamka jina lake, ambaye alimshika mkono na kumtaka waondoke eneo hilo.

“Walikuja watu wengi wanaume kwa wanawake, ghaflla walinizunguka na nikasikia kama kizunguzungu na akili yangu ikawa kama imezubaa,”alisema Shaban na kuongeza kuwa baada ya watu hao kumzingira walimwamuru aswage mbuzi zake na kuwarudisha nyumbani.

Ni hivi karibuni, Mji wa Geita na maeneo jirani ulikubwa na taharuki ya aina yake,pale mtoto Shabani Maulid (15) anaedaiwa kwamba alifariki dunia miaka miaka mitatu iliyopita, alipoonekana akiwa hai katika Kijiji cha 14 Kambarage, Mtaa wa Mbugani.

Tukio hilo lilizua hofu kwa wakazi wa Mji wa Geita huku waliowengi wakitaka kujua mtoto huyo aliyekutwa amefariki dunia baada ya kupotea kwa siku nne mwaka 2011 na mwili wake kuzikwa, inakuwaje leo hii anaonekana akiwa hai?

Tukio hilo lililotokea Septemba mwaka huu linashuhudiwa na wazazi wa Shaban, ndugu zake, jamaa na hata majirani wa eneo hilo ambao pia wanahoji, je aliyezikwa wakati mwili wa mtoto huyo ulipookotwa ni nani na je mwili wake uko kaburini au la?

Maswali haya na mengine, yalikosa majibu kwani baada ya kuonekana kwake, Shaban hakuweza kuongea vizuri na alionekana kutofahamu kabisa Kiswahili, lugha ambayo kabla ya kutoweka kwake aliifahamu vyema. Wakati huu mtoto huyu anaongea Kiha, japo nayo kwa tabu.

Hali hiyo iliwalazimisha wazazi wake kushirikiana na Jeshi la Polisi kumpeleka Haospitali ya Wilaya ya Geita ili apatiwe matibabu, lakini ni kama hawakuona mtoto wao akipata nafuu hivyo waliondoka naye na kuamua kumpeleka Kigoma Kambako anapatiwa tiba za jadi.

“Niliamua nimpeleke kwa waganga wa jadi huku nyumbani Kigoma na sasa hali inaendelea vizuri kwani anaweza kuongea japo ni kwa muda mfupi kisha hunyamaza”, alisema baba mzazi wa mtoto huyo, Maulidi.

Shaban alikuwa wapi?
Shaban hivi sasa anaendelea vizuri na ‘tiba’ anayopata huko Kigoma na aliweza kuzungumza na gazeti hili kwa simu, huku akieleza kutoweka kwake, pia huko alikokuwa kwa miaka mitatu, huku akiweka bayana kwamba hivi sasa anawatambua vizuri

wazazi na ndugu zake.
Alisema anakumbuka Januari 1, 2011 aliondoka nyumbani kwao na kuelekea malishoni kuchunga mbuzi, na wakati akiwa machungani ghafla lilitokea kundi la watu ambalo lilimzunguka.

Shabani anasema katika kundi hilo alikuwamo mwanamke ambaye hakumtaja kwa maelezo kwamba anashindwa kutamka jina lake, ambaye alimshika mkono na kumtaka waondoke eneo hilo.

“Walikuja watu wengi wanaume kwa wanawake, ghaflla walinizunguka na nikasikia kama kizunguzungu na akili yangu ikawa kama imezubaa,”alisema Shaban na kuongeza kuwa baada ya watu hao kumzingira walimwamuru aswage mbuzi zake na kuwarudisha nyumbani.

Maulidi alitoweka ghafla Januari 1, 2011. Wazazi wake wanasema siku hiyo aliondoka nyumbani asubuhi na kupeleka mbuzi malishoni, na kwamba siku hiyo hakurudi, jambo lililowatia mashaka wazazi wake hivyo kuamua kutoa taarifa polisi na kwa uongozi wa kijiji.

Taarifa za kupotea mtoto huyo zilienea kijijini hapo na ndipo walianza juhudi za kumtafuta na baada ya siku nne, alikutwa amekufa ndani ya kisima cha maji.

“Mtoto wetu aliondoka kwenda kulisha mbuzi siku ya sikukuu ya mwaka mpya muda wa saa nne asubuhi, hadi inafika saa 12 jioni hakuonekana na badala yake tuliona mbuzi wakiletwa na watoto wa majirani,”alisema Aziza Ramadhani mama mzazi wa Maulidi.

Aziza ndiye alikuwa wa kwanza kumtambua mtoto wake katika Mtaa wa Mbugani eneo la Majarubani na wakati huo alikuwa akitoka kwenye shughuli zake za kibiashara. Anasema alimwona Shaban akikatiza barabara.

“Nilimuona mwanangu akiwa anakatiza njiani ndipo nilimuita, Shabani mwanangu ni wewe? Niliposema hivyo alishtuka, nikaamua kumsogelea huku nikimwita jina lake ndipo alipoitika lakini hakunitizama usoni,” alisema mama huyo na kuongeza:

“Baada ya kuthibitisha kwamba ndiye, watu walijaa na ndipo kwa kushirikiana na majirani tulitoa taarifa polisi, na polisi wakaja kumchukua na kumpeleka hospitali huku akiwa haongei na tulitumia ishara kuwasiliana naye”.

Itaendelea wiki ijayo

Mwananchi

No comments: