Mbunge wa Iramba Maghariobi akiwatuliza wananchi wasiendelee kushangilia mafanikio yake aliyokuwa akiwaeleza hususani utekekelezaji wa Ilani ya CCM.Mwigulu Nchemba ametolea ufafanuzi wa Ujenzi wa Kituo cha kisasa cha afya kata ya Shelui wakati huo huo Mbunge huyo ametoa Gari la AMBULANCE kwaajili ya matumizi ya wananchi wa kata ya Shelui.
Kabla ya kutoa taarifa ya kuwapatia gari ya Ambulance kwaajili ya wagonjwa,Mbunge huyo amechangia mifuko 30 kwaajili ya ujenzi wa kituo cha afya na huku akitoa mabati zaidi ya miatano kwaajili ya ujenzi wa nyumba za Ibada na Vituo vya afya wilaya ya Iramba.
Naibu
katibu CCM Tanzania Bara na Mbunge wa Iramba Mgharibi Mh.Mwigulu
Nchemba leo jumapili 3/11/2013 amefanya mkutano mkubwa wa hadhara hapa
Iramba kata ya Shelui akizungumza na wananchi wake kuhusu shughuli
mbalimbali za maendeleo na kukabidhi madawati kwaajili ya shule pamoja
na kutoa taarifa ya kununua Ambulance kwaajili ya wanaShelui ya matumizi
ya kubebea wagonjwa kituo cha afya cha Shelui.
Mbunge huyo ambaye kwa muda mrefu sasa ameteka
media za nchi kutokana na umahili wake wa kisiasa,akiwa amembatana na
Mbunge wa Tabora Mjini amezungumza mambo mengi sana na wanashelui ikiwa
pamoja na kuwapa nafasi ya kuhoji na kuuliza maswali mbalimbali ya
mwendeo wa siasa na utekelezaji wa Ilani ya CCM.Mwigulu Nchemba
amewapongeza sana wakazi na wananchi wa Shelui kwa namna walivyoshiriki
kwenye ujenzi wa kituo cha afya ambacho yeye(mwigulu) amechangia mifuko
ya cement na mabati.Pia kwa sasa amewanunulia gari la Ambulance
kwaajilya wagonjwa,Gari lipo mbioni kuletwa Shelui mapema ndani ya Mwaka
huu.
kwa habari na picha zaidi bofya soma zaidi
kwa habari na picha zaidi bofya soma zaidi
Katika
hatua nyingine Mbunge huyo amewaomba Wanashelui kupuuzia kelele zozote
za wapinzai za kuhusu yeye,amedai kuwa wapinzani(CHADEMA) wameelekeza
nguvu zao kupambana na yeye kwasababu ni tishio kwao na amekuwa mstari
wa mbele kufichua maovu wanayofanya na kupanga kuyafanya.Hivyo yeye yupo
imara sana na anategemea wananchi wa Shelui hawatatoa nafasi kwa watu
waaina hiyo ya CHADEMA.Mwigulu amekwenda mbali zaidi kwa kusema kuwapa
nafasi wapinzani nikukaribisha vurugu,uvunjifu wa Amani katika kata
yao,Wapinzani ndani ya vyama vyao wanapigana ngumi mwenyekiti kwa
mwneyekiti na mmeona namna walivyosababisha kifo cha kijana pale
Ndago,walivyomwagia tindikali kijana(Musa Tesha)pale Igunga n.k.alisema
Mwigulu.
Vijana
endeleeni kujishughulisha na kazi za maendeleo,endeleeni kujikusanya
kwaajili ya kutoa misaada ya bodaboda na mikopo kama nilivyofanya kwenye
kata zingine,Naomba mshiriki kwenye michezo hasa hii michuano yangu
niliyoanzisha.Kukaa bila kazi ni hatari sana kwa kijana ndio maana
mnakuja kujiingiza kwenye vyama visivyo na mwelekeo wowote hapa
nchini"Mwigulu.
Jambo
kubwa la kufurahisha katika Mkutano huu Mh.Mwigulu Nchemba alitoa
nafasi kwa wananchi kutoa dukuduku zao,mawazo na maswali ya mambo
mbalimbali yanayowakabili.Maswali yote yalijibiwa na mengine kujibiwa na
watendaji moja kwa moja,Hatua hii imetoa fursa kwa wananchi kujua mambo
mengi hasa matumizi ya mfuko wa jimbo ambapo wengi wao walikuwa hawajui
kuwa Mbunge hakutani na fedha ya Mfuko wa jimbo zaidi ya Ofisi ya
waziri mkuu na mkurugenzi wa wilaya na kisha kwenda kwa mfumo wa cheki
kwenye serikali za vijiji.
Mengi zaidi tazama kwenye picha hapa chini.
Mwigulu Nchemba akishiriki kucheza ngoma ya asili ya kinyiramba na mmoja ya mwimbaji wa kundi la ngoma za asili hapa Shelui
Mh.Mwigulu
Nchemba akisalimiana na wananchi wake wa kata ya shelui hii leo kabla
ya kuanza kwa mkutano wa hadhara uwanja wa Shelui stendi.
Mh.Aden
Rage akishuka jukwaani mara baada ya kuongea na wananchi wa Shelui
kuhusu namna ya kutunza rasilimali watu walizonazo.Rage amewaomba
wananchi wa shelui kuhakikisha hawafikirii hata kumchagua mgombea yeyote
nje ya Mwigulu nchemba kwasababu ni Mbunge kijana mchapa kazi na mwenye
uwezo mkubwa wa kutatua matatizo ya wananchi wa Iramba na watanzania
kwa ujumla,Pia Mbunge huyo wa Tabora mjini na Mwenyekiti wa Simba Sport
Club ameweka bayana kuwa Ilani ya CCM imetekelezwa kwa kiwango kikubwa
sana hivyo haoni sababu ya Watanzania kufikiria kubadilisha serikali au
wabunge wa CCM waliopo madarakani.
Mh.Mwigulu nchemba akiwa na Mh.Aden Rage pamoja na diwani wa Shelui na mwenyekiti wa wanawake kata ya Shelui.
Kazi
ilikuwa kubwa sana kumuondoa Mh.Mwigulu Nchemba eneo la Mkutano
kutokana na umati mkubwa wa wananchi kutaka kumbeba na kusukuma gari
lake hadi eneo la barabara iendayo Igunga.
Mara
baada ya kumalizika kwa mkutano,Mh.Mwigulu Nchemba alipokelewa kwa mbio
na vigelegele toka kwa wananchi wake wa Shelui kumpongeza kwa namna
anavyowasaidia kutatua kero na shida mbalimbali zinazowakabili katika
shughuli zao za maendeleo.
CCM OYEEEEE!!!!
Msaada
wa kumuondoa eneo la mkutano linaendelea hapa kwa kusaidiana na
viongozi wengine wa CHAMA na serikali za mtaa hapa shelui ili
awezekuwahi ratiba zingine za kazi za maendeleo ndani ya jimbo lake la
Iramba Magharibi.
Hii
ni sehemu ya Mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye Mkutano wa hadhara
wa Mh.Mwigulu Nchemba kata ya shelui ndani ya jimbo lake la Iramba
magharibi.
Katika
hatua nyingine Mbunge wa Iramba Mh.Mwigulu Nchemba amekabidhi dawati 20
kwaajili ya shule ya msingi moja wapo hapa Shelui.Kwa dawati hizi 20
Mbunge huyo atakuwa amefikisha dawati 60 ambazo wananchi waliomba
kwaajili ya kutatua swala la watoto wao kukaa chini kwa kukosa
Madawati.Lakini pia Mbunge huyo amepeleka madawati zaidi ya 100 kwenye
shule mbalimbali ndani ya jimbo lake kulingana na mahitaji ya shule
husika.
Mtendaji
wa serikali ya Mtaa wa Shelui(kushoto) wakiwaonesha Wananchi moja ya
Dawati zuri na imara sana ambazo Mh.Mwigulu nchemba ametoa kwaajili ya
shule ya msingi hapa Shelui.
Kwenye
Mkutano huu wa hadhara.Mh.Mwigulu nchemba alitoa fursa kwa wananchi
wake kuuliza maswali mbalimbali yanayohusu mambo ya maendeeleo ndani ya
kata na jimbo lake la Iramba.Huyu ni mmoja wa vijana aliyejitokeza kutoa
shukrani zake kwa Mbunge wake kwanamna alivyomsaidia kutatua matatizo
yake na familia yake.Kijana huyu amewaomba wanashelui kutoa ushirikiano
wa kutosha kwa Mbunge wao kwasababu amekuwa bega kwa bega katika
kushughulikia matatizo yao.lakini pia kijana huyu alitumia muda wake
kuwaelimisha wananchi wa shelui kuwa na tabia ya kuhoji matumizi ya
fedha za Mfuko wa bunge na michango mbalimbali(mapato na matumizi).
Imekuwa
ni kawaida kwa wananchi kuogopa kuhoji namna fedha zao
zinavyotumika,Hivyo ni muda muafaka sasa kuwabana watendaji wa serikali
kutoa mapato na matumizi ya fedha za maendeleo ndani ya kata zao na
wilaya kwa ujumla.
Mh.Aden Rage na Mwigulu Nchemba wakisikiliza ukaribisho wa mwenyekiti wa Tawi wa chama cha mapinduzi(hayupo pichani),
Wananchi na Mbunge wao hapa Shelui wakimsindikiza kupanda gari.
Ilikuwa
ni furaha kwa Mwigulu nchemba kuzungumza na wananchi wake kuhusu
maendeleo anayowafanyia,Picha hii imepigwa wakati anacheza wimbo wa
kinyiramba kufurahia namna wananchi walivyojitokeza kwa wingi
kumsikiliza kwenye mkutano wake,.
Huu ni upande mwingine wa wananchi waliofika kusikiliza mkutano wa Mbunge wao Mh.mwigulu nchemba.
Mh.Mwigulu
Nchemba amewasisitizia sana wananchi wa Shelui na Iramba kushiriki
kwenye kazi za maendeleo,Kuachana kabisa na kumtegemea Mbunge kufanya
kila kitu.Pia amewaomba kuhakikisha wanasimamia kidete miradi mbalimbali
inayoendelea kutekelezwa ndani ya wilaya yake.Pia amewaomba vijana
kujitokeza kwenye chaguzi mbalimbali mwaka ujao kwenye serikali za
mitaa,Ameyasema hayo kwa kuzingatia kuwa sehemu kubwa ya wananchi wa
sasa ni vijana,hivyoi vijana wana fursa ya kushiriki kwenye kazi za
maendeleo kwa wingi sana,na endapo watashiriki kwenye chaguzi watakuwa
wamejiwekea mazingira mazuri yakuja kuwa viongozi wakubwa baadae.
Mh.Mwigulu
Nchemba akiteta jambo na Mwananchi wake akieleka kwenye jukwaa kwaajili
ya kuzungmza na wananchi wake wa kata ya Shelui.
1 comment:
TUWAFUNDISHE KUVUA SAMAKI BADALA YA KUENDELEA NA TABIA YA KUWAGAWIA VITOWEO, MAANA KWA KUENDELEZA TABIA YA MISAADA HATUWASAIDII WANANCHI WETU ZAIDI YA KUJENGA TABIA TEGEMEZI
Post a Comment