PICHA ZA MBEZI
Alex akipewa pole na Shangazi wa Martha
Kwa niaba ya Familia, Kamati ya Mazishi Marekani na Tanzania na ndugu na jamaa wote kwa ujumla tumeona ni vyema nanyi mkaona matukio yote kwani mlishiriki katika msiba huu. Mazishi yalifanyika Puma Sindiga siku ya Alhamisi ya Octoba 31, 2013. Video ya matukio yote Swahili TV Blog wataiweka soon.
picha zote kwa hisani ya Swahili TV Blog
Daniel Kalonga, DMK na Alex Dago
PICHA ZA AIPORT
Alex Kassuwi, Davis Mosha, Muddy na Masanja Mkandamizaji wakiusubiri mwili Airport, Dar es Salaam
Dada, ma wifi na Shangazi wa Marehemu wakiusubiri mwili kuwasili Airport, Dar es Salaam
DMK, Masanja, Joseph, Alex na Chris wakiusubiri mwili kuwasili Airport, Dar es Salaam
DMK, Alex na CEO wa DELINA GROUP (DGE) wakiusubiri mwili kuwasili Airport, Dar es Salaam
Ndugu, jamaa na marafiki walikesha Airport Dar kusubiri kupokea mwili Jumatano kuamkia Alhamisi ya tarehe 31, Oktoba 2013.
Kutoka kushoto waliokuwa majirani wa Martha Tanzania, Baba Mkwe, Kaka Isaya na Mjomba Kitundu wakiusubiri mwili kuwasili Airport, Dar es Salaam
Mara baada ya kuwasili kwa Mwili wa Mpendwa wetu Bi. Martha Shani, watu walishindwa kujuzuia na kuanza kulia hawaamini kama ni kweli yametokea.
Kaka wa Marehemu Bw. Noel Shani akiongoza njia kuelekea kwenye gari lililoandaliwa kuubeba mwili
Mtoto wa kwanza wa Martha na Alex, Joseph mwenye sneaker za Orange haamini yanayoendelea, akiwa amezungukwa na Mama zake wakubwa na wadogo
Joseph akipewa pole na Bibi yake mdogo huku DMK akiangalia
Ndugu, Jamaa na Marafiki wakiingia kwenye Coaster tayari kuelekea Singida Kwa Mazishi
SAFARI KUELEKEA SINGIDA
Martha Kilimba (Dada wa Martha), Daniel Kalonga na Mkurugenzi wa Swahili Media Int',MMK Media Group Bw. DMK wakiwa safarini kuelekea Singida kwa mazishi ya Mpendwa wetu Bi Martha Shani.
Martha, Freddy na Mwl. M. Kassuwi wakielekea Singida
Alex , Chris na Joseph Kilimba
DMK akiwa amechoka sana baada ya mikiki mikiki ya Safari na kukesha karibu siku zote za msiba
Jose Kilimba akishuka Dodoma kwa ajili ya Chakula cha Mchana
Bw. Alex akishuka Dodoma kwa ajili ya Chakula wakiwa Safarini Singida
Dada na Wadogo wa Bi. Martha Shani wakisubiri Chakula katika mapumziko mafupi Makao Makuu ya Tanzania Dodoma.
Kaka wa Marehemu wakipata chakula
Safari ya Singida haikupita muda ikaanza tena.
MWISHO WA SAFARI PUMA SINGIDA
Dada wa Marehemu Bi. Neema Shani alizidiwa sana na majonzi kiasi cha kuhitaji huduma ya kwanza mara kwa mara
Mama wa Martha waliosimama wa nne toka kushoto haamini kama ni kweli, alipigwa na butwaa na majonzi mazito sana.
Mama wa Marehemu Bibi Ruth Shani alishindwa kujizuia katika mchanganyiko wa uchungu na majonzi
Huwezi amini ni vigumu kuingia akilini mwake kwamba huyo aliyelala na Martha Shani R.I.P we love you so much Martha
Pumzika kwa Amani Martha tunakupenda Daima, hatujui ni kwa nini Mungu ameliruhusu hili jambo!
Mama Ruth Shani akimuaga mwanae kwa uchungu, majonzi na simanzi kubwa. R.I.P Martha
Mama Ruth Shani akimuaga mwanae kwa uchungu, majonzi na simanzi kubwa. R.I.P Martha
Mama Ruth Shani akilia kwa uchungu, majonzi na simanzi kubwa. R.I.P Martha we love you so much.
Mama mdogo wa Martha akimuaga mwanae kwa uchungu, majonzi na simanzi kubwa. R.I.P Martha
Bibi yake Joe na Chris akilia kwa uchungu R.I.P Martha Shani
Mama mdogo wa Martha aliyeketi na Mama yake Mzazi wakilia kwa uchungu R.I.P Martha
Mch. wa kanisa la Pentekoste Puma Singida akiongoza taratibu za ibada na mazishi
Pichani Kaka wa Martha wenye T shirt nyeupe wakisikiliza kwa makini
Mwenyekiti Kamati ya Mazishi Tanzania Bw. Hamis S, Mpinda akiongea machache
Kutoka kushoto; Mama mzazi wa Martha, na Mama yake mdogo wenye mavazi meupe
Mchungaji Peter Ihema wa Kanisa la Pentekoste Puma Singida akitoa Neno la Faraja kwa Ndugu,Jamaa na Marafiki
Kushoto; Mama mzazi wa Alex, Neema Shani (Dada wa Martha)
Mjomba wa Martha Shani, Bw. John Mbogo akitoa neno kwa niaba ya familia ya Wakwe wa Bw. Alex
Mh. Ramadhani Kulungu Diwani wa Puma akisema machache kuwafariji wafiwa,ndugu, jamaa na marafiki
Mama mzazi wa Alex Kassuwi wa pili toka kushoto waliokaa
Mchungaji Kijanga akiomba
Mama mzazi wa Martha Shani akimuaga mwanae kwa mara ya mwisho kabla ya kuelekea sehemu atayopumzika Martha mpaka hapo tutakapokutana tena baada ya hii Dunia.
Mama mzazi wa Martha akimuombea Martha
3 comments:
mhhh inauma saana poleni sana wafiwa imetugusa wengi kwa kweli, nilikua simfahamu lakini picha hizi zimeniliza tuendelee kumuombea apumzike kwa amani tuiombee na familia yake aliyoiacha hasa huyo mtoto mdogo mungu awatie nguvu mbarikiwe sana pole mama martha, poleni dada zake, bwana Alex pole sana,poleni kaka zake na familia yote tuko pamoja nanyi kwenye msiba huu mzito
poleni sana na msiba, nini kimemuongoa duniani dada Martha? kifo hiki ni kitendawili niliona picha wiki iliyopita mwenye kujua tunaomba mtuhabarishe aliugua au ni ajali? inasikitisha
pole sana Alex, it hurts, it hurts soo bad jamani. Mungu aendelee kuwatia nguvu,
Post a Comment