Aneth Kushaba AK47 akiongoza kikosi kazi cha Skylight Band kuwaburudisha mashabiki wake Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha maraha Thai Village Masaki jijini Dar, usikose usiku wa leo burudani kem kem bila kusahau staili yetu ya "Yachuma chuma" itachezeka.
Kipaji kipya ndani ya Skylight Band anatambulika kama Winfrida, binti mwenye kipaji cha aina yake njoo akurushe na ngoma kali za zamani zilizotamba enzi hizo kama Holiday iliyoimbwa na Madonna.
Aneth Kushaba AK47 na Winfrida wakitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band.
Kikosi kazi cha Skylight Band kikifanya yao jukwaani kwa mashabiki wake ndani ya kiota cha Thai Village sio ya kukosa jioni ya leo.
Mashabiki kwa raha zao.
Kipaji kipya ndani ya Skylight Band Winfrida (katikati) akifanya yake jukwaani huku akipewa support na Digna pamoja na Mary Lucos.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Sam Mapenzi a.k.a asali ya warembo akitoa burudani kwa mashabiki wake.
Shabiki mkubwa wa Skylight Band mdau Alois Ngonyani akiserebuka na burudani ya Skylight Band.
Baadhi ya mashabiki wa Skylight wakijinafasi kwa raha zao.
Mary Lucos akichizisha mashabiki wa Skylight Band.
Burudani inapokelea ni full kujiachia.
Shabiki aliyechizika na burudani ya Skylight Band na kuamua kupanda jukwaani kula sahani moja na waimbaji wa Band hiyo.
Hapa ni burudani mwanzo mwisho mpaka kieleweke.
Aneth Kushaba AK47 akiserebuka na shabiki wake nyimbo mpya inayobamba kila kona ya jiji inayoitwa SKELEWU kibao kilichoimbwa na msanii Davido ambapo kwa Skylight Band Sam Mapenzi anapiga miondoko hiyo LIVE...!
Palikuwa hapatoshi Thai Village.
Picha juu na chini mashabiki wa Skylight Band wakiburudika na mduara uliokuwa ukipomoshwa na Mary Lucos pamoja na Joniko Flower.
Mashabiki wakimwaga radhi.
Aneth Kushaba AK47 akijimwaga na shabiki wa Skylight Band.
Couples iliyobamba juma lililopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki.
Mdau Reginald Melecky akishow love na marafiki zake.
Aneth Kushaba AK47 akishow love na tajiri mtoto Eddie.
Mwanafamilia wa Skylight Band Victor Maginga akishow love mbele ya camera yetu.
Uzao wa BSS binti mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni Mary Lucas wa Skylight Band katika pozi.
Aneth Kusaba AK47 na Digna Mbepera wakiwa back stage katika pozi.
No comments:
Post a Comment