Peter Okoye
Kundi la P-Square ambalo limetua nchini tayari kwa show yao Jumamosi hii, limevitaka vyombo vya habari nchini hususan vituo vya radio na runinga kucheza zaidi nyimbo za wasanii wa nyumbani kwakuwa ukubwa wao (P-Square) barani Afrika ulitokana na vyombo vya habari vya Nigeria kuupa kipaumbele muziki wao.
Akiongea kwa msisitizo, mmoja wa mapacha hao, Peter Okoye alisema leo hii P-Square wanafanya show kubwa si tu barani Afrika, bali duniani kote na hujaza maelfu ya watazamaji lakini yote hiyo imetokana na mchango mkubwa wa vyombo vya habari vya nchini mwao.
“Wanamuziki wenu wanafanya kile kile sisi tunachokifanya, mnaowaona watu hawa hapa(Ben Pol, Profesa Jay na Lady Jaydee) mnaweza kuwafanya wawe wakubwa kuliko P-Square. Ukweli ni kwamba tunapromote muziki wa Africa. Waafrika huu ni muda wetu. Wamarekani nasema wanaogopa sasa hivi. Ningependa kuona mnaweka jitihada zaidi kwa wanamuziki wenu hapa. Nataka kuwaona wanakuja Nigeria na kuongoza concert. Hakuna mtu anayeza kufanya hivyo vizuri isipokuwa ninyi (vyombo vya habari),” alisema Peter.
“Wanaijeria walifanya hivyo kwetu, ninyi mnaweza kufanya kwa Jaydee, Profesa na wengine, kazi kwenu,” Paul alitilia mkazo.
No comments:
Post a Comment