Habari zenu ndugu. Kwanza napenda kumshukuru mwenyezi mungu anayetupa pumzi bila malipo, kwani yeye ndiyo kila kitu. Naishkuru familia yangu kwa kunipa moyo kila kukicha mpaka hapa leo hii. Napenda kutoa shukrani kwenu ndugu zangu kwa kunisapot katika kazi zangu na ushauli wa kila leo. Tunakutana na mitihani mingi sana lakini mungu anawapa moyo wa kuwa nami pamoja. shukrani sana kwa vyombo mbalimbali vya habari kwa mwaka mzima kuendelea kunisapot kwa kila hali. Radio na Tv mbalimbali kwa kutenga muda wa kupiga nyimbo zangu na kunipa interview juu ya kazi zangu. nawashkuru sana . Studio mbalimbali kwa kuweza kunipa nafasi ya kufanya kazi katika studio izo. Pia Bloggs na website na Magazeti mbalimbali, mmtenga muda wenu kwa kuthamini kazi za Dayna Nyange mmeonesha ushirikiano mkubwa sana kwangu. niwashukuru waandaaji wa matamasha kwa kunipa nafasi ya kufanya show katika matamasha hayo, ni jinsi gani mnavyoonesha kujali kazi zangu na kunipa moyo. Lakini pia watangazaji na ma dj wa Radio husika mmekuwa mkitenga muda wa kuwa nami katika kazi zenu,Niwashkuru sana Ma requester wote Tanzania na nje ya Tanzania kwa ku request nyimbo zangu na kupata nafasi ya kupigwa katika media izo. Nyinyi ni mchango mkubwa sana kwa sanaa yetu .Mafans wangu mnaozidi moyo na kunishauli juu ya kazi zangu na maisha kwa jumla kupitia vyanzo vyangu vya mawasiliano. Tunafunga mwaka 2013 na tunahamia mwaka 2014 Sitawaangusha.. Mwaka 2013 , tumepoteza ndugu zetu tuliokuwa nao ktk tasnia hii. Tuzidi kumuomba mungu azipumzishe roho zao mahali pema Albert mangwea, Langa kileo, marc malim Sharomilionea, Sajuki,na wengine wote wapumzike kwa amani. Nichukue nafasi hii kuomba radhi kwa wote niliowakosea au kukoseana kwani ni madhaifu ya kibinaadam. Lakini pia niseme tu kwa wote walionikosea Nimewasamehe bila kinyongo chochote na kwa dhati toka moyoni mwangu. Tusahau yaliyopita tuanze mwaka tukiwa Safi. Tumuombe mungu atupe afya njema na mafanikio zaidi mwaka 2014 na Kuendelea. Amina.
By
Dayna nyange
No comments:
Post a Comment