Mwanza, Tanzania. Gazeti la RAI leo katika ukurasa wake wa kwanza limeandika kwamba Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa amepigwa marufuku kukanyaga jijini Mwanza ambako chama hicho kimepanga kwenda kuwahutubia wananchi.
Mbali na kupigwa marufuku, viongozi wa Chadema wamepewa masharti ya kufanya kila linalowezekana kumrejesha madarakani aliekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe na wenzake waliovuliwa madaraka.
Viongozi wa Chadema wametakiwa kutekeleza agizo hilo ndani ya siku nne kuanzia jana.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Vijana wa Kanda ya Magharibi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Matawi ya Chadema, Mkoa wa Mwanza, Robert Gwanchele wakati akizungumza na waandishi wa habari. Kwa mujibu wa Gwanchele, yeye na wenzake wamelazimika kuchukua uamuzi huo kwa kuwa wanapinga kitendo cha kuvuliwa madaraka kwa viongozi hao kwa kuwa Chadema ilichukua hatua hiyo kinyume cha Katiba ya Chama hicho.
“Tutahakikisha tunawaondoa viongozi wote wa ngazi za juu kwa nguvu ya umma kwani Chadema siyo mali ya mtu binafsi, chama hiki ni cha wanachama.
“Hatutaki kuyumbishwa na watu wachache kwa maslahi yao binafsi, hao wanapaswa kukaa pembeni ili kupisha uchunguzi na kama hawataki kuondoka, nguvu ya umma itawaondoa na ndio maana sisi vijana wa Kanda ya Magharibi, tumeamua kuwapiga marufuku Mbowe na Dk Slaa kukanyaga Mwanza kwani wao wameamua kijijengea himaya isiyoguswa katika mikoa ya Kaskazini, sasa Mwanza wanakuja kutafuta nini,”amesema Gwanchele.
CHADEMA wamemtenda Zitto kama Malcom X alivyofanyiwa na Nation Of Islam hapa US. Wamemtumia kujenga chama hasa kupata wanachama pamoja na ruzuku kwani bwana mdogo ana charisma lakini mambo na maamuzi yote ndani ya chama yanafanywa kwa siri na yeye hausishwi. Kama kweli Zitto ni mwanasiasa mahiri basi apiganie wagombea binafsi katika katiba kwani sioni uhaini kuweka wazi kama unataka kugombea uenyekiti CHADEMA. Uhaini gani iwapo uchaguzi mkuu CHADEMA ni mwakani mwezi wa sita. Hapo naona wenzake wanamuweka sideline ili asipate nafasi kugombea uenyekiti na urais kupitia CHADEMA. Mbona CCM kila mtu kivyake katika mbio za kumrithi JK na hakuna anaeambiwa ni muhaini ndani ya chama. Siasa za bongo ni fitina mtindo mmoja. Wakiweka katika katiba hakuna vyama kupewa ruzuku tutaona kama kweli watu watakimbilia siasa.
ReplyDelete