ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, December 29, 2013

Jackie Cliff Amuachia Maagizo Ya Wosia Martin Kadinda …

Jackie Cliff Amuachia Maagizo Ya Wosia Martin Kadinda …

Baada ya kukamatwa na kilo 1.1 za heroin nchini China, mrembo Jackie Cliff kwa sasa anasubiria hatima yake kutokana na kosa hilo la kusafirisha madawa ya kulevya. Ikiwa nchini humo kuna adhabu tofauti za kuwahukumu watu wanao jihusisha na madawa ya kulevya.

Baadhi ya adhabu ni kifungo cha kuanzia miaka mitatu mpaka kumi na tano (3-15) na adhabu hii hutolewa katika mji wa Macau ambapo mrembo Jackie Cliff… Lakini kwa upande mwingine kuna adhabu ya kuhukumiwa kunyongwa au kifungo cha maisha katika miji mingine na pia hutegemea na aina za dawa za kulevya na uzito wa mzigo aliokamatwa nao mtuhumiwa.

Kupitia Personal Message ya BBM aliyoiandika mwana dada Jackie Cliff inayosema … ” Ikitokea nimekufa wosia Martin Kadinda ana maagizo ya nini cha kufanya … dnt ask pls.” inasemekana kuwa kama mrembo huyo atashindwa kujikwamua katika tatizo hilo basi, rafiki yake wa karibu ana maagizo yote ya nini cha kufanya kama yeye hatokuwepo tena.
Credit:GongaMix

No comments: