WABUNGE WA KAMATI YA MAHESABU YA SERIKALI (PAC) WALIOKO ZIARANI UK, LEO HII WAMETEMBELEA OFISI ZA SERENGETI UK NA KUJIONEA JINSI BOKSI LINYAVYOPIGWA.
WABUNGE HAO WAKIONGOZWA NA MWENYEKITI WAO MHESHIMIWA DEO FILIKUNJOMBE WALIJIONEA WENYEWE JINSI VIJANA WA KITANZANIA WAISHIO UK WANAVYOFANYA UKAGUZI WA MAGARI YAENDAYO AFRICA MASHARIKI NA PIA HUDUMA ZA USAFIRISHAJI WA MIZIGO.
ILIKUWA FURAHA KUBWA PALE CHRIS LUKOSI ALIPOKUTANA NA MHESHIMIWA ALLY KESSY MBUNGE WA NKANSI AMBAYE NDIE ALIEMPOKEA MIAKA 24 ILIYOPITA HUKO NKANSI RUKWA AMBAKO CHRIS LUKOSI ALIPANGIWA KIKAZI AKIWA JESHI LA POLISI, PAMOJA NA MENGI MENGINEYO, WABUNGE WALIFURAHI SANA KUONA JINSI WATANZANIA WAISHIO NJE (DIASPORA WANAVYOJISHUGHULISHA NA KUJITENGENEZEA AJIRA WENYEWE.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake