Kocha wa Makipa wa Simba, James Kisaka, yuko hoi kitandani, lakini amewaomba viongozi wa timu hiyo kumsaidia ili aiokoe afya yake.
Akizungumza nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam, Kisaka alisema hadi hivi sasa ameshatibiwa katika hospitali kubwa tatu za Muhimbili, CCBRT na Mwananyamala, Dar bila mafanikio ya kupona.
Kisaka alisema kwa sasa hawezi kutembea mwenyewe kutokana na hali yake mbaya kiasi cha kusababisha kuishiwa nguvu upande wa kushoto wa mwili wake ambapo hivi sasa anasaidiwa kutembea na mwanaye Christopher mwenye umri wa miaka saba pamoja na mkewe, Upendo.
“Hali yangu kama unavyoiona hapa siwezi kutembea mwenyewe, huu upande mmoja nikijaribu kutembea ni kama natetemeka hivi, nikijaribu kutembea kwa kujilazimisha ninaweza kuanguka, msaada mkubwa kwangu ni mwanangu huyu unayemuona na mke wangu.
“Sitaki kuonyesha naombaomba lakini nahitaji msaada wa viongozi wa timu yangu (Simba) na yeyote atakayeguswa na hili, nadhani sasa wakati huu ndiyo unaweza kujua wangapi walikuwa wanakuthamini, sichagui wa kunisaidia, yeyote atakayeguswa naomba anikimbilie,” alisema Kisaka.
SOURCE: CHAMPIONI
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake