Yaahidi kutinga Fifa kuisaidia Simba kuidai Etoile
Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) iliyokutana jijini Dar es Salaam juzi kujadili mambo mbalimbali yaliyofikishwa mbele yake ikiwamo usajili wa dirisha dogo, imebariki usajili wa Emmanuel Okwi kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga.
Aidha, kamati hiyo imezitaka klabu zenye matatizo ya usajili ikiwamo Simba, kuyarekebisha kufikia Januari 10, mwakani kabla haijachukua hatua zaidi.
Kadhalika TFF, imesema itaisaidia Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam kuhakikisha inalipwa Dola za Marekani 300,000 (Sh. milioni 480 za Tanzania) ambazo walistahili kuzipata kutokana na mauzo ya mshambuliaji wake wa zamani, Okwi, kwa timu ya Etoile du Sahel ya Tunisia
.
Okwi kwa sasa ametua kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga akitokea SC Villa ya Uganda.
TFF imetoa kauli hiyo kutokana na Simba kuweka pingamizi la usajili wa Mganda huyo ambaye ametua Yanga katika kipindi cha dirisha dogo na Desemba 21, mwaka huu aliichezea timu yake mpya kwenye mchezo wa kirafiki (Nani Mtani Jembe).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, ilisema shirikisho hilo litafuatilia fedha hizo ambazo Simba inaidai Etoile du Sahel katika Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Wambura alisema TFF inaamini Simba itapata haki yake kwa sababu ilikuwa ikimmiliki Okwi kihali kabla ya kumruhusu aichee Etoile du Sahel.
Baada ya Okwi kutua Yanga, Simba ililipa Dola za Marekani 5,900 Fifa ili iweze kupangiwa siku ya kusikilizwa kwa kesi yao hiyo ya madai.
Awali Etoile du Sahel ilikubali kuilipa Simba fedha za mauzo ya Okwi kwa awamu mbili lakini haikutekeleza makubaliano hayo.
Klabu hiyo ilieleza kwamba inakabiliwa na ukata kufuatia mechi zao kuchezwa bila mashabiki kutokana na machafuko ya kisiasa yaliyoikumba nchi yao mwaka jana.
Hata hivyo, viongozi wawili wa Simba, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hanspope na aliyekuwa Katibu Mkuu, Evodius Mtawala, walilazimika kwenda Tunisia kufuatilia malipo hayo na kuelezwa kwamba wangelipwa kabla ya mwishoni mwa Oktoba mwaka huu jambo ambalo halijatekelezwa hadi jana.
Mauzo ya Okwi ni moja ya sababu zinazowafanya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba na wanachama kutomuamini mwenyekiti wao, Ismail Aden Rage.
Lakini aliyekuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Mtawala, alilieleza gazeti hili kwamba fedha hizo bado hazijalipwa.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment