Mkurugenzi wa Kampuni ya Real Unique Tanzania, Bw. Albert Mkaoye ambao ndio waandaji wa Usiku wa Traditional Fashion Show akiwa kwenye red carpet na Mgeni rasmi MBUNIFU mkongwe wa mitindo na mavazi nchini, Asia Idarous Khamsin.
MBUNIFU mkongwe wa mitindo na mavazi nchini, Asia Idarous Khamsin, akiwa kwenye picha ya pamoja na wabunifu wa mavazi wanaochipukia Wancy na William.
MBUNIFU mkongwe wa mitindo na mavazi nchini, Asia Idarous Khamsin, na binti yake pamoja na wadau.
Wadau wakila pozi kwenye zulia jekundu.
Mkurugenzi wa Real Unique Tanzania Albert Makoye, akizungumza wakati wa kuwakaribisha wadau wa tasnia ya urembo nchini kwenye usiku maalum wa "Mavazi ya Kiutamaduni" ulioandaliwa na kampuni ya Real Unique Tanzania maalum kwa ajili ya kufunga mwaka ambao ulikutanisha wadau mbalimbali kwenye hoteli ya Regency Park Mikocheni jijini Dar.
Pichani juu na chini ni mbunifu wa mavazi anayechipukia Wancy akiwa kwenye picha ya pamoja na Models wa Real Uniuqe Tanzania waliovalia mavazi yake ya ubunifu.
Naibu Mkurugenzi wa Radio One, Bw. Isack Muyenjwa Gamba, naye alikuwa miongoni mwa wadau waliohudhuria onesho hilo.
Sehemu ya VIP kwa wadau wakishuhudia maonesho ya mavazi yaliyoandaliwa na kampuni ya Real Unique Tanzania kwa ajili ya kufunga mwaka.
Mgeni rasmi kwenye usiku maalum wa Traditional Fashion Show ulioandaliwa na kampuni ya Real Unique Tanzania, Mamaa wa Mitindo, Asia Khamsin Idarous akiwashangilia Skylight Band waliokuwa wakitumbuiza kwenye onesho hilo lililofanyika mwishoni mwa juma kwenye Hoteli ya Regency Park Mikocheni jijini Dar.
Skylight Band a.k.a habari ya mujini wakitoa burudani kwenye usiku maalum wa kufunga mwaka uliombatana na onesho la mavazi lililofanyika kwenye hoteli ya Regency Park jijini Dar.
Models wa Real Unique Tanzania wakipita jukwaani na vazi la ubunifu lililobuniwa na Mbunifu anayechipukia anayefahamika kwa jina la William.
Mbunifu anayechipukia akipita jukwaani na Models waliovalia mavazi yake katika onesho la kufunga mwaka la Traditional Fashion Show lililoandaliwa na kampuni ya Real Unique Tanzania.
Picha juu na chini ni Models wa Real Unique wakipita jukwaani na mavazi yaliyobuniwa na Mamaa wa Mitindo Bi. Asia Idarous Khamsin kwenye usiku maalum wa kufunga mwaka ulifanyika kwenye Hoteli ya Regency Park na kuandaliwa na kampuni ya Real Unique Tanzania.
MBUNIFU mkongwe wa mitindo na mavazi nchini, Asia Idarous Khamsin akipita jukwaani na Mmoja wa Models waliovalia ubunifu wake.
MBUNIFU mkongwe wa mitindo na mavazi nchini, Asia Idarous Khamsin, akitoa shukrani kwa kampuni ya Real Unique Tanzania inayolenga kuibua wabunifu wachanga ambao hawapati nafasi ya kuonyesha kazi zao kwenye maonyesho makubwa ya mavazi yanayofanyika nchini.
Models wa Kampuni ya Real Unique Tanzania waking'ara na mavazi ya Mamaa wa Mitindo Asia Khamsin Idarous kwenye pembezoni ya bwawa la kuogelea la Hoteli ya Regency Park, Mikocheni jijini Dar.
Models wakirudi kwenye chumba maalum mara baada ya kuonyesha kazi za wabunifu wa mavazi nchini.
Wadau wa tasnia ya urembo.
Mkuu wa Itifaki ya Kamati ya Miss Tanzania, Bw.Bosco Majaliwa akiwa na Naibu Mkurugenzi wa Redio One, Bw. Isack Muyenjwa Gamba.
Utu uzima dawa........MBUNIFU mkongwe wa mitindo na mavazi nchini, Asia Idarous Khamsin, akiserebuka na Skylight Band mara baada ya kumalizika kwa onesho la mavazi.
MBUNIFU mkongwe wa mitindo na mavazi nchini, Asia Idarous Khamsin, akishow love na baadhi ya Models pamoja na mbunifu wa mavazi nchini Martin Kadinda.
Bahati wa Atsoko Beauty and Cosmetics akishow love na Make Up artist anayefahamika kwa jina la Salum.
No comments:
Post a Comment