AT, Msanii wa muziki anayefanya vizuri hapa Tanzania, amewataka mashabiki wake kukaa tayari na ujio wake mpya ambapo katika kufungua mwaka mkali huyu amesema anatarajia kutoka na Cholo Ganun, mwanamuziki ambaye anashikilia rekodi ya kuwahi kufanya kazi na msanii wa kimataifa, John Legend.
AT amesema kuwa, kazi hii itakuwa ni yaina yake na yenye hadhi ya kimataifa kutokana na ujuzi wake yeye pamoja na Cholo, vilevile kazi ambayo inakwenda kwa jina Atentera ambayo kwa mujibu wa historia ya muziki wa AT, itakuwa ni kitu kipya na chenye mvuto kwa wapenzi wa muziki.
AT amesema kuwa mwaka 2014 ni wa kuungana wadau na mashabiki vilevile wasanii na kupeana sapoti ili kusaidia kuuvusha muziki mbali zaidi kwa manufaa ya wasanii, nchi pamoja na tasnia nzima ya burudani kwa ujumla

No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake