Sunday, January 19, 2014

CHOOMOOOO, KUMBIKUMBI HAO



Hiki ni kichuguu ambacho kimefunikwa kwa umahili kabisa, ambapo kote hakuna mwanga isipokuwa sehemu moja tuu.

Hili ni Tundu dogo maalumambapo kumbikumbi hawa hupumbazika na mwanga huu wakijua kuna mwanga ili watoke na ndipo wanapo kamatwa

Hii ni ndoo ambayo imetegeshwa katika Tundu dogo ambapo panatoka Mwanga , hapa ndipo kumbikumbi hawa wanapotokea na kudumbukia katika ndoo hiyo na hatimaye kushindwa pa kutokea




Picha hii inaonesha Jinsi kumbikumbi waliochanganyikana na Mchwa wakiwa wamedondokea katika Ndoo maalum ambayo hapa ni mtego wa kuwatega Kumbikumbi hawa.

Anaitwa Bwana Edward ambaye ni mtaalam wa kuandaa vichuguu hivyo, hapa alikuwa akihakikisha kama kweli kuna kumbikumbi hao.




Hii ni aina tofauti ya Kichuguu ambacho kimejitokeza pembezoni mwa shamba.

Huu ni aina nyengine ya mtego wa kumbikumbi hao



Hii ni Njia ambayo kumbikumbi hao wanakuwa wakitokea huku wakifuata mwanga watoke na kujikuta wapo mtegoni.


Juu ni vichuguu ambavyo bado havijatengenezwa , vikiwa vinaandaliwa kwa ajili ya kuwatega kumbikumbi hao..


Picha zote na Mbeya yetu blog

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake