Jamaa kagombana na mkewe.Kasusa kula,kurudi kazini kamkuta mkewe kavaa kanga imeandikwa"Ukisusa wenzio wala"ilipofika asubuhi mke kavaa kanga imeandikwa"ukitoka mwenzio anaingia"
Jamaa akagoma kwenda kanzini. Mke akavaa kanga imeandikwa "hamniwezi nimemzibiti ndio mana hatoki"Jamaa akaenda kuomba ushauri kwa rafiki yake akamwambia twende nyumbani.Walipofika wakamkuta kavaa kanga imeandikwa"ulizan rafiki yako kumbe adui yako". Kama wewe ndiyo mwenye boma hili utatatafuta tindikali au?.
Credit: Bossngassa

43 comments:
Kama mnasubiri kuolewa wanne mtasubiri sana na muache walale wenye raha zao
Wewe hapo juu utakuwa ni KIMBAUMBAU.Na mmeshakuwa watatu, wanne namtafutia mie.
Msonyooo! Katika wenye Raha na wewe Unajihesabu?Bora Ujinyamazie upate kustirika Ushuzi wewe.
kakwambia nani tutasubiri sana kwani wewe mungu muumba mbingu na dunia
subiri mumeo atakuja kuowa wanne ndo utakapojua kuku ni ndege au si ndege anamabawa na haruki so jiulize umme mmuumba wewe huyo mumeo au umezaa wewe
kwanza mumeo anachukuliwa kila leo ukiwa naye haishi kukufanya mjinga wake kwa kukudanganya kwamba ndo wewe peke yako kumbe mitaani wako wengi wake na kisha kuzalia wewe bado upo kwenye kizaaa pole bi dada mjinga raha unaijua wewe au ndo kujititimua tukuone unaraha kumbe roho yako iko juu na kuwaka waka kila leo
raha kuwa wanne ukiwa peke yako unadanganywa usisikiye kaa jitulize umestirika tulia usijigambe mungu si mjinga leo anaweza akakugeuzia kibao na ukaletewa hao wanne na wala usiwe na la kufanya zaidi utajiachisha na ukawe maali ya umma
sadakta maneno haya ya kanga na awe anawatimizia wote haki zao kwa sawa hapo ndo raha iliyoje other wise anajitafutia madhambi ya bure na uhasama na wakezeee
mumeo kama utamzuia asiowe akakusikia basi si mumehuyo ukae ukijua anapinga amri ya mungu na la pili na wewe pia si mkee kama kweli mtoto wa kiislamu hakuna chako peke yako katika dunia hii bora ukubali ku shara na wenzako kuliko na walio mabarabara usio wajua kaa utafakari wewe unaye jiona unalala na kula raha zako na wala si raha hujui kama anaye pembeni au vipi
wanne bora niachike sitaki kurogwana na hao wakezake na stress za kijinga jinga
mummy usijigambe ukaona uko naye hujui anapotoka ndani ya nyumba huko kazini,mitaani anaye nani usijigambe mummy tuliza ball raha jipe mwenyewe katika ulimwengu wa leo
bi dada mlele hivyo hivyo na kumhudumia badala ukiacha hivyo anaoa mwinginewe kishakuona umekufa kimapenzi kwake lakini kaa ukijua kwamba ana plan ya kuowa wa pili mpaka wa nne ndugu wameshamshauri hili sema yuko na wewe kwa vile unamhudumia na kumtuza na yeye pesa zake anaziweka kwa wa pili pole bi dada usijigambe haupo peke yako raha na wa pili pia anaipata tena sana
si mwanamke mwenzako ndo maana yupo na wewe mmoja angekuwa kibeberu kweli angeweza kuwa na hao wanne lakini si kibeberu si rijal ndo maana yuko na wewe na wala si muuislamu ni muislamu wa jina tu na wala hajui uislamu wake akiujua atakuongezea timu ndani ya nyumba na achacharuke ndo sifa ya mwanamme rijal mwenye ndevu kinywani
dj luke umezua balaa bwana kwa hii kanga acha bwana watu wanatoa comment kama wanasesere
nimependa kanga hii je wapi nitaipata wadau niambiyeni please
mwanamme mwenye siha yake na mwenye uwezo basi si vibaya awe na wanne wakina mama mruhusuni jamani msiwe wachoyo wa kukaa peke yenu
dawa ya kuwakomesha wanawake wajeuri unamuoleya wanne na kila mmoja anatia akili zake na pia unawastiri waliokuwa hawajaolewa mungu humbarik mwanamme mwenye wake wengi someni dini mtalione hilo
Ndio kwanza mnaiona hii kanga mbona ya mwaka jana. Subirini muone nyingine wote mtashangaa.nitawapa example
KWIKWIKWIKWIIII HII KHANGA KIBOKO IMENITULIZA NAFSI YANGU! UUUWIIII USHUZI JASHO LAMTOKA. LAZIMA NIIAGIZE BONGO.DJ LUKE UNAVISAA WEWE ILA ASANTE KWA KUTUSTARESHA NA MAUCHOVU YA SCHEDULE.
tunasubiri mdau kwa hamu kubwa hiyo kanga inginewe kumbe dunia ina mambo sikudhani wala kutegemea katika dunia hii nitakuja kuona kanga yenye maneno kama haya wakina mama isikurusheni roho poeni roho zenu ni kanga tuu anayekupenda kaanaye salaama
hivi watu wanapata nafasi wapi ya kuandika maneno kama haya kama tuko manzense uwanja wa fisi au jangombe what a shame and a waste
walioshadidia maneno ya kifedhuli wote watakuwa wake wenza wana beef na walio kuwa na mume aliye na mkee mmoja na wala hashughuliki na mwingine nakusupport sister wa mwanzo watasubiri sana wakitaka kuwa wakee wanne.
mungu ndo mpangaji na mtoaji wanne si vibaya lakini kama mume hajaamua msimuamulize ameridhika na huyo mmoja na ni kidume cha shoka kweli
Makurumbembe yanatiririka nimeshasema mtasubiri sana wengine hapo meno yanangoka bado tu hata wa salamu hakuna mtabaki hivohivo ooh tuolewe wanne haaaaa napita njia mimi
Waacheni wazae nje walezi si mpo? Lakini nasemaje ndoa no hatutaki mibanano wakati wa kulala weraa weraa jiwe limerushwa gizani
Maneno ya wakosaji hayooo raha uwe peke yako babu
KANGA NYINGINE:1 Lala nikukande,ukilegeza nikupande 2: Taarisha mambo nipenyeze mtaimbo 3: mengi yatanishinda ila nitakukata kizinda
Please print some example I send those are the ones with no MATUSI BUT I have KANGA UKISHA SOMA UTANYAMAZA
Mmh marekani hii wanaume hawana uwezo wa wawili huyo mmoja basi msaidiane maisha. Wenye waume kelele za mwewe zisiwatishe wataishia ivo ivo kutamani waume wa wenzao. mimi nasema msemo ni 'Mkisubiri wa wenzenu mtasubiri sana' kaka luke tia huu msemo haloooo
Tiririkeni mpaka povu la midomo liwatoke lakini ukweli ni tuacheni turare wenye raha zetu poleni na baridi
Kiruu kama huna mwenza yaani uko single nendeni tu pokono lodge mkapumzike watu wanataka kushelekea valentine mambo ya wawili wawili
Hahhahaaaa KIMBAUMBAU Hataki kusikia wanakuwa wanne haaaaa Uwiiiii!!!! Sasa sibora muwe wanne ili upumzishe Mgongo maana Umeshaanza kuongezewa mijelli ya mgongo bora upate Msaada wa nyumba ndogo.
TUTABANANA TU HIVYO HIVYO SILVER SPRING. HAHAAA USHUZI LAZIMA MUWE WANNE. UTAKE USITAKE ILI UNENEPE KIDOGO HUMUWEZI PEKE YAKO MDENGELEKO HUYOO OOOOOH SHAURI YAKO UNAHITAJI MSAADA KESHA KUVUJISHA JELLY YA MGONGO KIFATACHO MUNGU ANAJUA. JIWE LIMETUPWA KIZANI. MBAVU ZANGU MIE.
Mtabaki hivo hivo mngekua waolewaji mngekua na waume tayari halooooo jiwe limerudi gizani valentine inakuja jamani mambo wawiri wawiri
Wenye wivu wajinyongeeeeee watu wako kwao na raha zao jamani laha ya mume aijuae mke
You all have issues. Where are your husbands when you are looking for them. FYI: with the other woman and you know it.VALENTINE IS COMING AND HALF OF YOUR HUSBANDS WILL BE WITH THE OTHER WOMAN FIRST OR LAST.IS THE TRUTH.Nyamazeni
Wewe kama bwana wako anacheat sio kila mtu anatabia hiyo wanaume wengi tu wametulia na wake zao na mifano tunayo nxt time tafuta bwana wa maana aspend valentine n wewe utakua na kinyenyea wacheni wivu na ndoa za watu
Mnachekesha kweli hao wanaume kwani hawana macho au akili mpaka muwapangie waongeze wake? Wameridhika na wake zao na wewe mwenye experience ya bwana zako kucheat inabidi uende unyagoni ukafundwe. Bwana ukijua kumridhia hafurukuti wala haoni cja pembeni. Jumuiya fungueni darasa la kufunda watu wazima ovyo
Uuuuuuwi Mdau hapo juu utakuwa Kimbaumbau bora ungeandika tu Kiswahili ndugu yangu maana umejiaibisha sio OTHER WOMAN IS OTHER WOMEN HAHAHAAAAA!!!!!! half of your husbands?????? what the hell!!! Rudi Darasani Mbio ukakimalizie Kizungu ulichokikimbia maaana Nomaaaaa.
Tutokee sie uko huna mpya! kakucheat na kakwambia live hadi baba mtu kaja kusuruhisha wewe bora ukubali tu amuoe muwe wanne otherwise utaendelea kukonda Ushuzi usiwe mbishi midawa haifanyi kazi tena, Dawa ni kuolewa wanne ili apate kutuliza hasira.Mchele mmoja Mapishi mbalimbali Ushuzi wewe, Mdengeleko wa watu kachoka kula wali wa maji, Mapishi huyawezi wape jiko atape kulishwa biliani hahaaaa utaliaje leo. Kitendawili chako hicho Kimbaumbau.
Kimbaumbau kijiti hata hamueleweki kajipumzisheni pocono jibanzeni kwenye miti mpige picha hata ndani hamuingiagi jamani valentine hiyooo wawiliwawili ka kawa ma mtuache miaka 100 na waume zetu haloooooo mawe yanarushwa tu gizani kidesign
Hizi safari za kutembeza vizee park halafu mnavipa camera vitupige picha tuacheni hahahaha basi na mada ifungwe hao wanaume na waoe watu watulie. Nawaalika harusi ya kakangu anaoa virginia katoto kadogo details zitarushwa sooon vijimambo luke naomba uwe dj
Wewe mdau wa6.43 unachekesha kweli neno biriyani liana kushinda kutamka eti biliani kwa Hali hii utasubiri sana kua mke wa pili hahahahah movie yetu inaendela yenu mikanda imejaa endelea ni kupaparika mtaa wa pili kiruuu
Hahaaaa KIMBAUMBAU Maskini siri zako zipo nje nje muache tu amuoe maana hasikii haoni kwa mtoto S. UBISHI NDIO HUWA UNAKUPONZA MUACHE MDENGELEKO APATE JIKO LA MCHINA KACHOKA NA JIKO LA KUNI HAHAAAAAAA KICHEKO CHAKO HICHO. WEWE ENDELEA TU KUBISHA UTAMU WA NDOA KUSHEA HASWA MKIWA WANNE BURUDANI ROHO YAKE ACHAGUA TU WAPI KWENYE SHUKA JIPYA MDENGELEKO WA WATU ANAPUNGUZIA STRESS ZAKE. HAHAHAHAH JIWE LIMETUPWA NA KUMAPATA MLENGWA KWENYE PAJI LA USO CHALI KWA STRESS HAHAAAAAA. NIMEIPENDA SAAAAANA HII KANGA. DJ LUKE WEWE KWELI KIBOKO.
lazima amuoe upate kulijua jiji huna mbele wala nyuma analalamika kila kukicha kwa Mchumba wake wa nje. Ndio maana anafanya kazi bila Off anakukimbia wewe Kimbaumbau umekwishaaa.Hahaaaa akufukuzae hakwambii toka, bora Umuache aoe atakuwa na furaha na atasahau kama kakuchoka akitoka kufurahishwa na wewe utachekewa japo kidogo.
Kimbaumbau ndio nani jamani?. Twambieni nasisi tumjue
Post a Comment