Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic akizungumza na mchezaji anayetaka kumsajili Mserbia Ilic Milos (kushoto) wakati alipokutana nae kwenye Uwanja wa Amaan mjini Unguja
Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic amesema atahakikisha wachezaji wawili wa kigeni wanaongezwa kwenye kikosi chake msimu ujao kama akiendelea kukinoa kikosi cha 'Wanamsimbazi'.
Akizungumza na NIPASHE mjini Unguja juzi kabla hajaanza safari ya kurejea Dar es Salaam juzi asubuhi, Logarusic aliwataja wachezaji hao kuwa ni winga wa kulia wa Tusker FC ya Kenya, Ali Abondo na beki Mserbia anayecheza pia kama kiungo, Milos Ilic wa URA ya Uganda.
Alisema wawili hao wanacheza soka la kiwango cha juu amewafuatilia kwa miaka zaidi ya mitatu.
"Abondo alikuwa mchezaji wangu wakati nikiinoa Gor Mahia mwaka jana, amejiunga na Tusker FC hivi karibuni. Milos pia namfahamu vyema. Kama nitaendelea kuwapo Simba, itabidi tuangalie uwezekano wa kuwapata ili kuimarisha zaidi timu," alisema Logarusic ambaye amepewa mkataba wa miezi sita na Simba baada ya kujiunga na klabu hiyo baada ya kutimuliwa kwa Abdallah 'King' Kibadeni Desemba mwaka jana.
Milos (25) alijiunga na URA Agosti 22 mwaka jana na ameichezea mechi 10 akifunga bao moja. Alitokea benchi kipindi cha pili na kung'ara katika mechi yao ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Simba waliyopigwa 2-0 kwenye Uwanja wa Amaan kisiwani Unguja Januari 10.
Hata hivyo, ndoto za kocha huyo kuwasajili wakali hao huenda zikagonga mwamba kutokana na Kanuni za Ligi za Shirikisho la Soka (TFF) kutorusu idadi kubwa ya wachezaji wa kigeni kusajiliwa na timu za ligi kuu nchini.
Kuanzia msimu ujao timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, zitalazimika kuwa na wachezaji wa kigeni wasiozidi watatu ili kutekeleza maamuzi ya Azimio la Bagamoyo la 2007.
Kwa sasa Simba ina wachezaji watano wa kigeni ambao ni mabeki wa kati Gilbert Kaze (Burundi), Donald Mosoti (Kenya) na Joseph Owino (Uganda), kipa Yaw Berko (Ghana) na mshambuliaji Amisi Tambwe (Burundi).
Azimio la Bagamoyo pia linakataza timu za ligi kuu kuwa na makipa wa kigeni, hivyo klabu hiyo ya Msimbazi italazimika kutomwongeza mkataba kipa Berko baada ya huu wa sasa kumalizika Mei mwaka huu.
"Nafikiri waliopitisha suala hilo (Azimio la Bagamoyo) wamelenga kuwabeba wachezaji wa ndani pasipo kuangalia madhara yake. Timu za Tanzania zitafanya vibaya kwenye mashindano ya kimataifa," alisema Logarusic.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment