ANGALIA LIVE NEWS
Tuesday, January 14, 2014
PAMBANO LA CHEKA NA MRUSI HATIHATI
Pambano la Francis cheka na bondia toka rusia ambalo linalotangazwa kufanyika mwezi ujao February lina mashaka makubwa kufanyika kwake kutokana na muandaaji wa pambano hilo jay msangi ndie aliyemleta phil wiliams toka marekani na kumpiganisha na cheka bila ya kumlipa na madai bado yanaendelea huku jay akikwepakwepa, wakati siku hiyo ya pambano la cheka na williams timu ya matibabu ikiongozwa na dr donald madono haikulipwa gharama zao huku marefa na majaji pia hawakulipwa pesa yoyote jambo linalotishia pambano hili na mrusi kwa kuwa majaji wote wa ngumi hawapo tayari kufanyakazi na mtu asiyeeleweka wala sio mwaminifu, ukiachilia mbali hayo hakuna bondia hata mmoja kati ya waliotangazwa watacheza utangulizi ambaye amekwisha sainishwa mkataba wa kucheza mchezo huo na hata wengine hawana taarifa yoyote kama kuna mashindano yanayomkabili ni jambo linalosababisha mabondia kulalamika kutumiwa majina yako kwa manufaa ya watu wengine.kama jay atalipa madeni aliyobakiza na kulipia ushuru wake anashauriwa awasainishe mikataba ya uhakika mabondia anaowahitaji mbele ya mwanasheria au kituo cha polisi cha kati(central police station).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment