Wednesday, January 15, 2014

YANGA YAMKARIBISHA KOCHA MPYA KWA KUTOA KIPIGO CHA BAO MBILI MTUNGI

Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga wamemkaribisha kocha wao mpya kwa ushindi wa mabao 2-0 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Altay SK leo.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Viwanja vya hoteli ya Sueno Beach Side, mabao yote ya Yanga yalifungwa kipindi cha pili.
Huku Kocha Hans Van Der Pluijm akishuhudia, Didier Kavumbagu alikuwa wa kwanza kuandika bao kabla ya Emmanuel Okwi kufunga la pili katika dakika ya 57.
Timu hiyo ua daraja la pili nchini Uturuki ilionyesha ushindani zaidi ingawa Yanga walikuwa na kazi kupita wao tokea kuanza kwa kipindi hicho.

Hiyo ni mechi ya pili mfululizo ya kirafiki, Yanga inabuka na ushindi baada ya kushinda mechi ya kwanza kwa mabao 3-0

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake