ANGALIA LIVE NEWS

Monday, February 17, 2014

BRUNA MARQUEZINE: BEAUTIFUL ONYINYE WA KIBRAZIL ALIYEMMWAGA NEYMER NA MAMILIONI YAKE

Bruna Marquezine: Mrembo wa Kibrazili aliyemwaga Neymar na mamilioni yake

KWELI pesa si kila kitu. Haiwezi kununua mapenzi. Aliyekuwa mchumba wake anamiliki pato la Dola 20.5 milioni, lakini hilo halikuwa na maana kwa mrembo wa Kibrazili, Bruna Marquezine, ambaye kipato chake kizidishwe mara 30 ndiyo afikie kiwango cha mwanamume huyo.
Mrembo Bruna hakutazama nyuma na kuamua kumpa kisogo mwanasoka Neymar, ambaye pia ni Mbrazili mwenzake.
Kwa pesa anazopiga staa huyo wa Barcelona, wengi waliamini isingekuwa rahisi kwa mrembo Bruna kuacha kuitumia nafasi hiyo ya kuponda raha, lakini haikuwa hivyo. Sasa binti huyo amechukua njia zake na kuamini kwa nguvu zake atapiga pesa za kutosha, hivyo hana haja ya kumtegemea mtu.
Bruna Marguezini, ambaye jina lake la awali ni Bruna Maia Reis, alizaliwa Agosti 4, 1995 mjini Duque De Caxias, Brazil. Anatajwa kuwa na kipato cha Dola 700,000.
Jinsi alivyopata pato hilo
Kazi yake kubwa ni uigizaji na kutamba kwenye sinema mbalimbali nchini Brazil kumemfanya kuingiza kipato hicho. Kitu kilichompa sifa kubwa na kumpatia dili mbalimbali za kucheza sinema ni uzuri wake. Bruna anatajwa kuwa mwigizaji mrembo zaidi nchini Brazil.
Filamu yake ya kwanza ilikuwa Gente Inocente, ambayo ilimpa umaarufu mkubwa na kumfanya awe na pesa. Pia binti huyo ameng’ara kwenye vipindi mbalimbali vya televisheni zikiwamo tamthilia.
Bruna pia amekuwa akishiriki masuala ya mitindo na mashindano ya kudansi kwenye televisheni ambayo yanamwongezea kipato. Umahiri wake kwenye filamu umemfanya kushinda tuzo 11 kuanzia mwaka 2003.
Bruna alianza kuigiza akiwa na umri mdogo na alionekana kwenye matangazo mbalimbali ya biashara na video za muziki. Alipofikisha umri wa miaka minane alipiga hatua muhimu baada ya kuonekana kwenye kipindi mashuhuri cha televisheni nchini Brazil kilichokuwa kikiongozwa na Xuxa.
Baada ya kufanya vizuri hapo, mvuto wake ulimfanya apate dili za kucheza tamthilia na televisheni yake ya kwanza kutamba nayo ilikuwa ‘Rede Globo’. Baada ya hapo akaendelea kutesa kwenye ‘America’, ‘Cobras e Lagartos’, ‘Deseo Prohibido’ na ‘Negocios en China Araguaia’.Kitu kilichompa umaarufu Bruna ni ubora wake kwenye filamu. Kazi hiyo inampatia pesa na ndiyo maana aliona kitu cha kawaida tu kumtema staa mwenye pochi la nguvu na kisha akaendelea na maisha yake.
Baadhi ya filamu alizocheza mrembo huyo ambaye zimempatia pesa nyingi na dili za matangazo ya kibiashara ni pamoja na ‘Sitio do Picapau Amarelo’, ‘Mulheres Apaixonadas’, ‘Xuxa Especial de Natal’, ‘Negocio da China’, ‘Xuxa Abracadabra’ na ‘Xuxa e o Tesouro da Cidade Perdida’.
Aachana na mpenzi wake
Mapenzi si pesa, hicho ndicho unachoweza kusema baada ya mrembo huyo kuamua kumtema supastaa Neymar mwenye pesa za nguvu.
Mrembo huyo aliamua kufuta picha zote alizopiga na Neymar katika mitandao ya kijamii jambo ambalo lilifichua wazi kwamba mapenzi ya wawili hao yaliyodumu kwa mwaka mmoja hayapo tena.
Bruna, ambaye kwa sasa anatamba kwenye tamthilia ya ‘Em Familia’ inayoonyeshwa katika kituo cha Globo, uvumi wa yeye kuachana na Neymar ulizagaa tangu Desemba mwaka jana kabla ya kila mmoja kusherehekea Mwaka Mpya kivyake.
CREDIT MWANASPOTI

No comments: