-Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi M.K Tarishi akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu, kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Ruvuma Bw. Severin Tossi Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi M.K Tarishi akihutubia wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Utamaduni na Kumbukizi ya Vita ya Majimaji katika ukumbi wa Songea Club,kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Bw Joseph.J. Mkirikiti na kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw Severin Tossi. Philip Maligisu, Mhifadhi Kiongozi Makumbusho ya Majimaji akitoa maelezo kwa wajumbe katika eneo ambalo lilikuwepo kanisa katoliki la kwanza nchini.
HOTUBA YA KATIBU MKUU, WIZARA YA MALIASILI NA UTALII, BI. TARISHI M.K WAKATI WA UFUNGUZI WA MAADHIMISHO YA UTALII WA UTAMADUNI NA KUMBUKIZI YA VITA YA MAJIMAJI TAREHE 25 FEBRUARI 2014, UKUMBI WA MALIASILI, MJINI SONGEA-RUVUMA
Awali ya yote, nichukue fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kuifikia siku ya leo. Ninayo furaha kubwa kupewa heshima ya kuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa maadhimisho haya muhimu kwa historia ya nchi yetu. Nimefurahi kwa sababu hii imekuwa ni fursa kubwa na ya pekee kwangu kukutana na kufahamiana na wadau wa urithi wa utamaduni kutoka Kanda ya Kusini hususan mkoa wa Ruvuma. Kupitia fursa hii, nitapata nafasi ya kubadilishana uzoefu nanyi wadau wetu muhimu mnaotusaidia katika jukumu la kuhifadhi, kulinda, kuendeleza rasilimali za urithi wa utamaduni na utalii katika ukanda huu wa Kusini.
Ndugu wageni waalikwa na wadau wetu, Nimefurahishwa pia na utaratibu huu wa wadau kukutana na kujadili namna ya kuendeleza utalii wa utamaduni na kuenzi mchango wa Mashujaa wetu wa Vita ya Majimaji. Utaratibu huu ni mzuri kwa sababu unatekeleza Sera na Sheria zetu ambazo zinaelekeza ushirikishwaji wa wadau katika kuhifadhi na kuendeleza kumbukumbu za kihistoria na kutunza maeneo ya urithi wa utamaduni. Aidha, napenda kuwakumbusha kuwa sote kwa ujumla wetu tunawajibika kuuenzi kwa kutambua na kutumia kiundelevu urithi wa utamaduni uliopo katika maeneo yetu. Kila mdau anayo nafasi katika kuendeleza na kuimarisha rasilimali hizi kwa manufaa ya Taifa letu
No comments:
Post a Comment