Na Steven Augustino wa demashonews, Tunduru
SERKALI imewaahidi walimu kote Nchini kuwa itawalipa Madai yao yote
mwaka huu zikiwa ni juhudi za kuinua na kuongea ari ya utendaji wa
walimu hao na kuyafikia malengo iliyojiwekea ya matokeo makubwa sasa
(BRN).
Kauli hiyo ilitolewa kwa nyakati tofauti na
Mafunzo ya Ufundi Mwl. Jenista Mhagama wakati akiongea na walimu
katika shule za Msingi Tuwemasho, Matemanga Sekondari na Kiuma Bonite
Sekondari Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma na kuongeza kuwa tayali
Wizara yake imeomba Shilingi Bilioni 61 ili zitumike kulipia madeni
hayo.
Akifafanua taarifa hiyo Mwl. Mhagama alisema kuwa halai hiyo imetokana
na Serikali kusikia kilio cha muda mrefu amvacho kimekuwa kikitolewa
na Walimu hapa nchini hali amabayo iliisukuma kutuma wataalamu wake
kufanya uchunguzi wa kero hizo nakubaini uhalisia wa madai hayo.
Alisema kufutia hali hiyo kuanzi sasa walimu wanapaswa kuwajibika
katika ufundishaji na kuahakikisha wanamaliza Mitaala na vipindi
walivyo pangiwa ili kuongeza ufaulu kwa watoto waliopewa mamalaka ya
kuwalea.
Sambamab na hali hiyi pia Mwl. Mhagama aliwagiza maafisa elimu Wilaya
kutoka ofisini na badala yake waende Mashuleni kusikiliza Kero zinazo
wakwaza walimu huku akiwataka maafisa wa Tume ya Utumishi wa Umma
(TSD) kuwafuatilia na kuwachukulia hatua Walima wazembe na watoro
kazini.
Akizungumzia anguko la elimu katika Wilaya hiyo,kushuka kwa taaluma
kwa wanafunzi kuliko sababisha kuwepo kwa wimbi kubwa la Wanafunzi
wasiojua Kusoma,Kuandika na Kuhesabu Naibu waziri huyo alisema kuwa
hivi tayari Wizara kupitia wataalamu wake imejipanga kwa ajili ya
kuanzai kuifanyia marekebisho Mitaala ya Elimu, kuandaa utaratibu wa
kutoa mafunzo maalumu kwa walimu wawili kutoka kila Shule nchini ili
watakapo maliza waende kufundisha watoto wa madarasa ya awali zikiwa
ni juhudi za kuwajenga watoto kujua msingi huo.
"serikali kupitia Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi imejipanga
kufanya na kugalamia mafunzo kwa Walimu Wawili kutoka kila Shule hapa
nchini zikiwa ni juhudi za kuinua taaluma kwa watoto wetu" alissitiza
Mhagama.
Naibu waztri uyo yupo katika Ziara uhamasishaji wa maendeleo ya Elimu
ya siku 8 Mkoani Ruvuma akiwa anatokea katika Mikoa ya dar es salaam,
Lindi na Mtwara zikiwa ni siku 16 toka ateuliwe kushika wadhifa huo
ambao yeye anadai kuwa kama ni upele umepata mkunaji kwavile
anayafahamu fika matatizo, kero na vikwazo vya utendaji kazi za walimu
hapa nchini.
No comments:
Post a Comment