ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, March 8, 2014

ANGALIA MAZOEZI YA MWISHO YA YANGA KABLA YA KUIVAA AHLY NA ALICHOKISEMA KOCHA


Yanga imefanya mazoezi ya mwisho kabla ya kuivaa Al Ahly leo kwenye Uwanja wa Max jijini hapa.
Mazoezi yamefanyika kwenye Uwanja wa Max jijini hapa. Mazoezi hayo yalifanyika usiku.


Yalikuwa mazoezi mepesi na Kocha, Hans van Pluijm alisema ni kwa ajili ya kuupima uwanja.Wachezaji waliopo nchini Misri na kufanya mazoezi ya mwisho leo jioni ni"

Magolikipa: All Mustafa "Barthez", Juma Kaseja, Deogratias Munish "Dida"

Walinzi: Juma Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, David Luhende, Kelvin Yondani "Cotton", Nadir Haroub "Cannavaro"

Viungo: Haruna Niyonzima, Saimon Msuva, Athuman Idd "Chuji", Frank Domayo "Chumvi", Nizar Khalfani

Washambuliaji: Mrisho Ngasa, Said Bahanuzi, Emmanuel Okwi, Hamis Kizza, Jerson Tegete na Didier Kavumbagu 

Mechi itachezwa kuanzia majira ya saa 1kamili kwa saa za Misri sawa na saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, na kesho wapenzi, wadau na wanachama wa Young Africans watapatiwa link ya kuweza kutazama mchezo huo moja kwa moja kwa kutumia internet.

Mungu Ibariki Young Africans, Mungu Ibariki Tanzania .
Jiji la Alexandria 
Hotel ya Sheraton waliyofikia Yanga

No comments: