ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 27, 2014

FAINALI YA KUMTAFUTA ‘MWANAMKE WA MWAKA’ KUFANYIKA DODOMA JUMAMOSI

Meneja Mkuu wa kampuni ya Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho, akielezea mchakato wa kumpata 'Mwanamke wa Mwaka' utakavyokuwa. Kushoto ni Mratibu wa Matukio wa Global Publishers, Luqman Maloto.
Abdallah Mrisho akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu tukio hilo.Wanahabari wakiwa kazini.
Luqman Maloto akisistiza jambo kwenye mkutano huo.
KAMPUNI ya Global Publishers Ltd ambao ni waandaaji wa shindano la kumtafuta mwanamke bora wa mwaka ambaye mchango wake wa maendeleo kwa jamii umewazidi wenzake, imethibitisha fainali hizo kufanyika keshokutwa Jumamosi.
Akizungumza na wanahabari kwenye Hoteli ya Atriums, Jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Abdallah Mrisho, amesema fainali hiyo itafanyika mjini Dodoma ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye atawakabidhi tuzo washiriki wanne walioingia fainali na kumkabidhi tuzo maalum mmoja kati yao aliyewazidi wenzake alioingia nao fainali.
Washiriki walioingia fainali ni Prof. Anna Tibaijuka, Dk. Asha-Rose Migiro, Anna Kilango Malecela na Dk. Maria Kamm.
(PICHA : RICHARD BUKOS / GPL )

No comments: