Huwezi
kuamini lakini ndo ukweli hii ni mojawapo ya barabara ya mtaa wa Uhuru
uliopo maeneo ya Mwenge ikiwa imejaa maji baada ya mvua kunyesha leo
mchana lakini kikubwa cha kujua ni kwamba maji haya ni maji ya mvua na
hata maji taka maana chemba nyingi eneo hili zilikuwa zikitoka maji hayo machafu.
Mmoja
wa wasamalia wema aliamua kuwapandisha wanafunzi kwenye Toyo yake ili
kuwavusha kwenye eneo la barabara lililokuwa limejaa maji mengi eneo la
Maghorofa ya JWTZ yaliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
Gari likipita kwa shida kwenye barabara ya mtaa wa Uhuru baada ya mitaro ya eneo hilo kuzidiwa na kupelekea maji hayo kuanza kupita kwenye barabara hiyo
Baadhi ya wananchi wakivuka kwa kupita kwenye maji hayo yaliyojaa barabarani
Unaweza
kusema ni mto lakini eneo hili ni barabara iliyobadilika kwa muda mfupi
baada ya mvua kunyesha eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam
Magari yakipita kwa shida kwenye barabara baada ya maji kujaa barabarani
Mojawapo ya chemba ya maji machafu iliopokaribu na ofisi za TRA ya Kinondoni ikiwa inatoka maji machafu baada ya mvua kunyesha kwenye eneo hilo na kuingia mtaroni.
PICHA NA PAMOJA BLOG
1 comment:
Hapa ndipo tunapochanganyikiwa Dar es salaam kodi za pango , bei za viwanja , kodi za maegesho ya ni ghali Sana lakini miundo mbinu ni mibovu na wala hakuna anaekuna kichwa kutafakari zaidi ya kujaza matumbo ya wachache kutokana na kodi:( Jiji linakusanya kodi za maegosho ya magari kila kona mjini , kodi za biashara hazigusiki ..Jamani hizi barabara hata mawaziri siwanapita pia au ndiyo kazi ya Mungu? Kuwajibika si utamaduni wetu..Posta mpya imegeuka bwawa:( jaribu kufungua biashara uone kama hautalipia kodi kama uko New York:(
Post a Comment