Mwanamuziki wa Injili aliyetokea kwenye familia ya kidini Milka Kakete anasema alianza kuujua na kuufahamu muziki kwa kina tangu akiwa mdogo, kwani familia yake ni ya kikristo na amepata malezi ya kuwa karibu na kanisa siku zote.
Milka ambaye ni mkazi wa Canada na familia yake akiwa ni mama wa watoto watatu na familia yake anaeleza kuwa anaipenda sana familia yake na anajaribu kuweka sawa maisha ya familia na uimbaji wa Injili.
Hivi karibuni alitembelea idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika (VOA) hapa Washington Dc na kupata nafasi ya kufanya mahojiano na idhaa hiyo , Milka ameeleza mengi ikiwa ni pamoja na jinsi alivyoanza kuimba, nafasi yake katika jamii na familia na pia kueleza vipaji vyake vingine alivyojaliwa na Mungu ikiwa ni pamoja na ushauri wa masuala ya ndoa.
Alipoulizwa juu ya uchungaji Milka alicheka na kusema huo sio wito wake ila yeye anamtukuza Mungu na kueneza neno lake kwa nyimbo za Injili halikadhalika kutoa ushauri kwa wanandoa.
Sikiliza wimbo wake wa Injili nakung'ang'ania kwa kubofya hapa.
[audio http://sundayshomari.files.wordpress.com/2014/02/milka-nakungangania.mp3]
Milka Kakete pia alifanya mahojiano na VOA kusikiliza mahojiano hayo bofya hapa.
http://www.voaswahili.com/content/article/1866954.html
Video vya Nakung'ang'ania.
http://youtu.be/UL_YBJIGals
No comments:
Post a Comment