ANGALIA LIVE NEWS
Tuesday, March 4, 2014
SHUKRANI
BALOZI FULGENCE MICHAEL KAZAURA (11/9/1940 – 22/02/2014).
RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE, APUMZIKE KWA AMANI AMINA!
KWA NIABA YA FAMILIA NZIMA YA MAREHEMU BALOZI FULGENCE MICHAEL KAZAURA PAMOJA NA NDUGU ZANGU WOTE TUNAPENDA KUTOA SHUKRANI ZETU ZA DHATI KWA WANA DMV KWA MIOYO YENU YA UKUNJUFU KWA KUJITOA KWENU KWA HALI NA MALI KUANZIA SIKU YA MSIBA ULIPOTOKEA KUJA KUTULIWAZA NYUMBANI WAFIWA NA PIA KUJUMUIKA NASI KANISANI KWA AJILI YA MISA YA KUMUOMBEA MAREHEMU BABA YETU ILIYOFANYIKA KANISANI MT. CAMILLUS, SILVER SPRING - MARYLAND TAREHE MACHI 1, 2014.
KWA UPENDO MLIOKUWA NAO KWETU MLIWEZA KUACHA AU KUAHIRISHA SHUGHULI ZENU NA KUJA KUJUMUIKA NASI, HATUNA CHA KUWALIPA ILA MUNGU PEKEE NDIYE ANAYEWEZA KUWALIPA KWA UPENDO WENU MLIOTUONYESHA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU.
MWENYEZI MUNGU AWABARIKI SANA.
AHSANTENI SANA!!!
WENU,
SIMA KAZAURA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment