Loveness Mamuya anatoa shukurani kwa wote wanaDMV na Watanzania wengine nje ya DMV waliomsapoti kwenye kipindi hiki kugumu cha kumpoteza dada yake ambaye alikwenda Tanzania kwa miezi 3 akimuuguza lakini Mwenyezi Mungu amempenda zaidi na jina lake lihidimiwe.
Pia anapenda kuushukuru uongozi wa CCM DMV na kwengineko kwa salamu za rambirambi walizomtumia asanteni sana na Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema awazidishie.
Shukurani za pekee kwa marafiki zangu wa karibu walikua karibu na mimi siku zote usiku na mchana wakinifariji katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na dada yangu ambaye nilimpenda sana lakini Mwenyezi Mungu amempenda zaidi. Sina cha kuwalipa kitakacholingana na yote makubwa mlionifanyia yote namwachia Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema awazidishie maradufu. Asanteni.
1 comment:
Shukran zimefika dada yangu loveness tuko pamoja, mungu akupe nguvu. DULLAHZAY
Post a Comment