Na Jovina Bujulu
Suala la Jinsia katika uongozi wa Bunge Maalum la Katiba limeibua Mjadala mzito katika nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa bunge hilo.Mjumbe wa Bunge hilo Lediana Mung’ong’o ndiye aliyekuwa wa kwanza kuibua suala hilo wakati wa mjadala kuhusu marekebisho ya kanuni za bunge kipengele 8(i) kinachozungumzia utaratibu wa kumchagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti.Mung’ong’o alitaka kipengele hicho kuzingatia uhusiano wa kijinsia, ambapo kama mwenyekiti atakuwa ni mwanaume, makamu wake awe mwanamke au kama Mwenyekiti atakuwa mwanamke, makamu wake awe mwanaume.“Mwenyekiti hili suala la Mwenyekiti na Makamu wake hatuna budi kuangalia suala la jinsia kwamba ikiwa mwenyekiti atakuwa ni mwanaume, makamu wake awe mwanamke au kama Mwenyekiti atakuwa mwanamke, makamu wake awe mwanaume” alisema Mung’ong’o.Naye Mjumbe wa Bunge hilo Anna Abdalah alisema kuwa suala hilo lilikosewa Tangu awali hivyo hakuna budi makubaliano yafanyike kwa busara maana wanawake wenye sifa na uwezo wapo wengi Tanzania Bara na Zanzibar.Akichangia katika suala hilo Mjumbe wa Bunge Hilo ambaye ni Naibu Waziri Wizara ya Fedha Adam Malima alisema kuwa ili kuwepo kwa amani na Mshikamano sheria haina budi kusema wazi endapo Mwenyekiti atatoka Tanzania Bara basi Makamu wake atoke Zanzibar.
Akijibu hoja hiyo Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Othman Masoud Othman alisema kuwa suala hilo liwe la marekebisho lakini si kwa kuvunja sheria hiyo.
“Sharti hilo likibadilishwa litakuwa ni kituko na tutakuwa tunarekebisha sheria ambazo hazikutungwa na Bunge Maalum la Katiba hivyo ni busara kufanya makubaliano ili kufikia muafaka wa jambo hilo” alisema
Othman Masoud Othman.
No comments:
Post a Comment