Mkurugenzi Mkuu, Idara Kuu ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa anayeongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 45 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa, akifuatilia kwa makini hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo wa wiki moja Unaofanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kati ya nchi 24 ambazo ni Wajumbe wa Kamisheni hiyo. Mkutano wa Kamisheni ulifunguliwa na Bw. WU HONGBO, Katibu Mkuu Msaidizi anayeongoza Baraza la Umoja wa Mataifa la Uchumi na Maendeleo ya Jamii ( ECOSOC) Katika Hotuba yake Bw. HONGBO ametoa changamoto kwa wataalamu hao wa Takwimu ya kuhakikisha kwamba wanafuatilia kwa karibu majadiliano yanayoendelea kuhusu ajenda mpya za maendeleo endelevu baada ya 2015 kwa kile alichosema, utekelezaji wa malengo hayo utahitaji kuungwa mkono na takwimu rasmi na endelevu.
Na Mwandishi
Maalum
Wajumbe
wanaohudhuria Mkutano wa 45 wa
Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa
Mataifa, wamepewa changamoto ya kuhakikisha kwamba, Takwimu rasmi na sahihi zinaunga mkono pamoja
na mambo mengine, utekelezaji na
usimamizi wa Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu ( SDGs) baada ya 2015.
Changamoto hiyo imetolewa siku ya Jumanne na Katibu Mkuu
Msaidizi Bw. WU HONGBO anayeongoza
Baraza la Umoja wa Mataifa
linalosimamia masuala ya Uchumi na Maendeleo ya Jamii ( ECOSOC). Bw.
HONGBO alikuwa akifungua rasmi mkutano wa wiki moja wa wajumbe wanaounda Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa
Mataifa.
Wajumbe hao ni kutoka nchi 24 ikiwamo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ujumbe
wake katika Mkutano huu unaongozwa na
Dkt. Albina Chuwa, Mkurugenzi
Mkuu wa Idara Kuu ya Taifa ya Takwimu.
Bw. WU HONGBO amewaeleza wataalamu hao wa masuala ya Takwimu
kwamba, mwezi wa Tisa mwaka huu, Umoja wa Mataifa, utaandaa mikutano kadhaa
ya kilele, ukiwamo Mkutano wa Tatu wa Kimataifa kuhusu maendeleo
ya mataifa ya visiwa vidogo.
Ni katika
kipindi hicho hicho pia ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,
amewaalika Wakuu wa Nchi na Serikali, wafanyabiashara, vyama visivyo ya kiserikali, na watu wa kada
mbalimbali kuhudhuria mkutano wa kilele
kuhusua masuala ya mabadiliko ya Tabia
nchi.
“ Hivi sasa kuna mchakato unaoendelea
wa majadiliano ya wazi ya Kikundi Kazi kuhusu ajenda mpya za Malengo ya Maendeleo Endelevu baada ya 2015 ( SDGs). Majadiliano haya na mengine , ni wazi kwamba nafasi na mchango wa Takwimu ni muhimu sana katika kuchangia na kutoa mwongozo
wa uundaji wa serĂ¡ na uundwaji wa kamati za ufuatiliaji wa utekeleazaji wa makubaliano
yatakayofikiwa” akasisitiza Katibu Mkuu
Msaidizi
Katika
kuhakikisha kwamba, wataalamu
hao kutoka Taasisi za Kitaifa za Takwimu
wanafuatilia kwa karibu mikutano
mbalimbali muhimu
inayoendelea katika Umoja wa Mataifa, yakiwamo majadiliano ya Kikosi Kazi kuhusu
Maendeleo Endelevu baada ya 2015.
Katibu Mkuu Msaidizi, Bw. HONGBO amesema, wakati
mkutano huo wa Kamishieni ya Takwimu ukifanyika, katika ukumbi mwingine, kulikuwa kukiendelea majadiliano ya awamu ya tisa kuhusu maendeleo endelevu baada ya 2015.
“ Wiki hii inatoa fursa ya aina yake kwenu, pamoja na ajenda mbalimbali
zinazowakutanisha hapa, na wakati
huu mkiendelea na mkutano wenu, kuna mkutano unaoendelea kuhusu maandalizi ya malengo
mapya ya maendeleo. Itakuwa vema na ni matumaini yangu kuwa mtaitumia fursa hii kuwasiliana na kubadilishana
mawazo na wajumbe wenzenu wanaohudhuria mkutano huo. Lengo likiwa ni
kuhakikisha kwamba malengo hayo mapya ya
maendeleo endelevu utekelezaji wake unaungwa
mkono na Takwimu rasmi na endelevu” akasisitiza.
Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ni kati ya nchi 30 ambazo ziliteuliwa kushiriki katika
majadiliano ya Kikosi Kazi kuhusu
maandalizi hayo ya SGDs baada ya 2015.
Katika mzunguko
huu wa tisa wa majadiliano wa hayo kuhusu SDGs,
Tanzania inawakilishwa na Dkt.
Lorah Madete, Afisa Mkuu na mchambuzi wa
Sera kutoka Ofisi ya Rais, Kamisheni ya Mipango.
No comments:
Post a Comment