Ofisa wa Polisi anayeshughulikia Dawati la Jinsia na Watoto, Afande Kasusura akiwa na bwana Majaliwa ambaye ni mmoja wa watuhumiwa wa ubakaji.
Majaliwa akitolewa ndani ya nyumba wanayoishi ambayo ndiyo iliyotumika kuwabaka watoto hao.Mtuhumiwa namba moja Sebastian Mashauza aliyewarubuni wanafunzi wake akiwa chini ya ulinzi mkali.
KATIKA jambo ambalo limevuta hisia za wanafunzi wengi na walimu wa Chuo cha Mwenge, ni tukio lililotokea jana majira ya jioni katika Chuo cha Mwenge kilichopo Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
Kwa mujibu wa mzazi wa watoto wanaotuhumiwa kubakwa ni kwamba tukio zima lilitokea Ijumaa iliyopita majira ya jioni ambapo binti yake (jina linahifadhiwa) mwenye umri wa miaka 15 ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Maki iliyopo Olele huko Marangu Kitowo alitoweka nyumbani kwao Marangu Kitowo.
Mwanafunzi huyo alitoweka akiwa na mwenzake (pia jina linahifadhiwa) mwenye umri wa miaka 16 na hawakuweza kuonekana mpaka Jumapili jioni.
Baada ya kuonekana ndipo walipobanwa na kueleza kuwa walikuwa Moshi Mjini kwa mwanaume ambaye alikuwa ni mwalimu wao shuleni na anasoma Chuo cha Mwenge.
Baada ya maelezo ya watoto haO, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wazazi wa watoto hao ndipo walipofika katika chuo hicho na kuweza kuwatia mbaroni wanafunzi hao Sebastian Mashauza mwenyeji wa Kigoma ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza na mwenzake aliyetambulika kwa jina moja la Majaliwa mwenyeji wa Kigoma na ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo hicho.
Mmoja wa wanafunzi waliofanyiwa unyama huo, akizungumza na mwandishi wa habari hizi, alisema anamtambua Sebastian Mashauza kama mwalimu wake aliyekuja shuleni kwao akifundisha somo la Kiswahili. Baada ya mwezi mmoja aliondoka wakawa wanawasiliana kwa njia ya simu na siku ya Ijumaa mwalimu huyo akamtumia shilingi 10,000/= kwa njia ya M-Pesa ili aje mjini na akamwambia aje na mwenzake ndipo alipomuomba rafiki yake amsindikize.
Wakiwa kwa mwalimu huyo, ulipofika usiku, mwalimu akamshawishi walale na kumshawishi mwenzake alale na rafiki yake aitwaye Majaliwa.
Mwanafunzi huyo alizidi kueleza kuwa, walipotaka kuondoka siku inayofuata hawakupewa nauli ndipo ikapelekea walale tena mpaka siku ya Jumapili walipopewa nauli na kuondoka kurudi nyumbani.
Hata hivyo uchunguzi wa awali umebaini kuwa, Sebastian Mashauza, alifundisha katika shule ya Maki Sekondari anayosoma mmoja wa wanafunzi hao na alikuja kama mwalimu wa 'Field' kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Kwa sasa watuhumiwa wako Kituo cha Polisi cha Marangu tayari wakisubiri utaratibu wa kisheria kukamilika kabla ya kupelekwa mahakamani.
(Chanzo na Kilimanjaro Blog)
2 comments:
KWANZA KABISA HAO WABAKAJI NA WASHAWISHI SI WALIMU TENA. WAMEPOTEZA SIFA ZOTE ZA KUWA WALIMU SABABU MWALIMU MWEMA NI MLEZI WA WANAFUNZI KAMA MZAZI NAMBA MBILI.
PILI WAPEWE ADHABU KALI ILI KUWAFUNDISHA NA WENGINE WENYE TABIA KAMA HIZO.
TATU.....WANAFUNZI NAO MMEZIDI KWA KUPENDA URODA MKINGALI WADOGO. MKOME KABISA KWA UMALAYA, MLIDHANI HIYO M-PESA NI BURE?
Jamani hizi habari za kisheria inabidi zichunguzwe kwa makini kabla hazijatangazwa.
Sasa hao mabinti walipopokea nauli na kusafiri kukutana na wanaume walikuwa wanafikiria nini? Na huyo shahidi hajanukuliwa popote akisema walibakwa. Ni kwamba tu walicheleweshwa kuondoka.
Inasikitisha.
Post a Comment