Kesi
ya mwanariadha wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius Jumanne hii imeendelea
kwa siku ya pili ambapo shahidi wa pili wa upande wa serikali amesema
alisikia sauti za juu usiku alipouawa mwanamitindo Reeva Steenkamp.
Oscar akiwa ameziba masikio yake wakati ushahidi ukiendelea kutolewa
Kama
alivyosema shahidi wa kwanza, Estelle van der Merwe anayeishi jirani na
Pistorius ushahidi wake nao ulikinzana na maelezo ya mwanariadha huyo
kuwa haikuwa ‘sahihi’ na sio sawa kusema kuwa alikuwa na ugomvi na
mpenzi wake kabla hajafa.
Oscar akiwa analia wakati wa kesiyake ikiende
Van
der Merwe ameiambia mahakama hiyo kuu ya North Gauteng mjini Pretoria
kuwa alishindwa kulala mida ya saa 8 usiku kutokana na kelele za watu
waliosikika wakigombana.
Awali
shahidi wa kwanza, Michelle Burger, alisema kuwa alisikia mwanamke
akipiga kelele kuomba msaada, baadaye akasikia sauti ya mwanaume ikiomba
msaada kabla ya milio ya bunduki kusikika.
Katika
hatua nyingine Oscar Pistorius alilia kwa uchungu mahakamani humo baada
ya wakili wake kudai kuwa Reeva Steenkamp aliumia vibaya kwenye ubongo
na hivyo haikuwa rahisi kupiga kelele.
Advocate Barry Roux alitoa maelezo hayo kufuatia ushahidi wa jirani yake aliyedai kusikia kelele baada ya milio ya bunduki.
Hata
hivyo kesi hiyo ilikatizwa katikati na jaji kuamuru kufanyika
uchunguzi wa kwamba kituo kimoja cha runinga cha Afrika Kusini kilikuwa
kikionesha picha za shahidi – kinyume na amri ya mahakama ya mashahidi
kutooneshwa.
No comments:
Post a Comment