Kupitia blogu yake, Mjumbe wa Bunge la Katiba, Salma Said ametoa ufafanuzi wa kilichotokea leo Bungeni na mustakabali wake kama ifuatavyo:
Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samuel Sitta amelazimika kuakhirisha kikao hadi Jumatatu ambapo kabla ya kusikilizwa taarifa za kamati nyengine mbili zilizobaki itabidi Mjumbe wa Bunge hilo Tundu Lissu aendelee kutoa
ufafanuzi wake ambao aliuanza leo kabla ya kukatika kwa matangazo hayo.
Mwenyekiti wa Bunge hilo alilazimika kusitisha shughuli hizo baada ya
Mjumbe Freeman Mbowe kutoa taarifa za kupokea kwa kukatika kwa matangazo
huku baadhi ya wajumbe wengi wakiwa wametumiwa sms katika simu zao wakitaarifiwa kwamba matangazo hayo yanayorushwa moja kwa moja kupitia TBC hayapo hewani.
Mwenyekiti alimtuma Katibu wake Yahya Khamis kwenda kusikiliza
kinachoendelea na hatimaye kuja na taarifa kwamba ni khitilafu
iliyotokana na hali mbaya ya hewa huko Dar es Salaam ambapo kuna mvua
tokea juzi.
Hata hivyo, baadhi ya wajumbe walipingana na uamuzi huo wakihoji ni kanuni gani inayosema kuwa kwa kuwa matangazo yamekatika ndiyo bunge liakhirishwe lakini Mwenyekiti alijibu kwamba kanuni inamruhusu Mwenyekiti kuchukua maamuzi ambayo anaona yanafaa na kutumia busara, hivyo yeye ametumia busara kutokana na kuwa mjadala wa katiba muhimu kusikika na Watanzania wote.
Hata hivyo, baadhi ya wajumbe walipingana na uamuzi huo wakihoji ni kanuni gani inayosema kuwa kwa kuwa matangazo yamekatika ndiyo bunge liakhirishwe lakini Mwenyekiti alijibu kwamba kanuni inamruhusu Mwenyekiti kuchukua maamuzi ambayo anaona yanafaa na kutumia busara, hivyo yeye ametumia busara kutokana na kuwa mjadala wa katiba muhimu kusikika na Watanzania wote.
Kwa umuhimu huo, ili watu wengine wasije kuona kwamba matangazo hayo
yanakatwa kwa hujuma au kuwanyima haki wengine na kuwapa fursa wengine,
ameamua kuchukua uamuzi huo ili kila upande uweze kusikika huko nje na
umma wa Watanzania na khasa kwa kuzingatia tayari kuna mkataba kati ya
Serikali, Bunge na Shirika la Utangazaji (TBC) kwamba wataonesha live
shughuli za majadiliano katika Bunge Maalumu la Katiba. Hivyo basi
wananchi walikataa kuendelea na mjadala huo hadi hapo matangazo hayo
yatakaporudi na ndiyo Mwenyekiti akatumia busara kuliakhirisha Bunge
hadi Jumatatu.
Juzi wakati akitoa ufafanuzi ya maoni ya wajumbe wachache Professa Ibrahim Lipumba pia matangazo hayo yalikuwa yakikatika katika jambo ambalo limekuwa likiwasumbua wananchi wengi ambao wanaofuatilia mjadala huo wa katiba na hivyo kiasi cha baadhi ya wananchi kujenga dhana kwamba hali hiyo husababishwa kwa makusudi ili kuwakosesha wananchi wasisikie maoni kutoka kwa wapinzani ambao wana haki sawa kama wanachama wengine ambao wanahitaji kusikiliza hoja za pande mbili.
…tutaendelea tena inshallah Jumatatu ambapo watakaotoa ufafanuzi ni kamati mbili zilizobaki ambazo ni Freeman Mbowe na Ismail Jussa, baada ya Wenyeviti kuwasilisha maoni ya Wajumbe wengi na wachache.
Wajumbe wa Bunge Maalum la KatibaTundu Lissu( kushoto) akisalimiana na Profesa Ibrahim Lipumba (katikati) mara baada ya kikao cha Bunge hilo leo mjini Dodoma. Kulia ni Mchungaji Peter Msigwa. |
No comments:
Post a Comment