Sisi
watanzania wa Washington DC, Maryland na Virginia pamoja na vizazi vyetu
tunapenda kutoa pongezi kwa Serikali yetu ya Tanzania kwa Mchakato mzima wa
Katiba mpya unaoendelea.
Tunapenda
Kutoa Tamko Rasmi kwa Bunge la Katiba na Serikali kutoa haki ya Uraia kwa
Watanzania Wote popote walipo Duniani. Uraia Wa Mtanzania aliezaliwa Tanzania na
Kizazi chake usijali hali na mahala alipo Mtanzania Huyo.
Kutokubaguliwa
kwetu kwenye swala hili la Haki ya Kuzaliwa na Kuruhusiwa kwa Uraia Pacha kwa
Waliozaliwa Tanzania na Vizazi vyao ni muhimu katika kuimarisha nchi, kutoa
haki kwa Watanzania wote waliozaliwa Tanzania pamoja na vizazi vyao. Haki ya
kuzaliwa kwa watanzania wote kutaimarisha
Zaidi mahusiano kati ya watanzania tulio nje na serikali yetu tukufu.
Watanzania
Hapa Washington ,
DC na tulio nje tumekuwa mbele kuitangaza nchi yetu, kuiwakilisha nchi yetu na
kuibeba Bendera ya Tanzania
huku nje . Watanzania tumekuwa tukishirikiana na Viongozi wa nchi yetu wanapokuja
huku nje kwenye mambo mbalimbali ya kimaendeleo, kijamii na kielimu ili
kuhakikisha nchi yetu inasonga mbele.
Watoto
wetu waliozaliwa huku nje wamekuwa wakiimba nyimbo ya Taifa la Tanzania
wanapokuja viongozi mbali mbali huku na kwenye shughuli mbali mbali za kitaifa
na kimataifa ambazo huwa tunaiwakilisha nchi yetu huku ugenini.
Watanzania
wenye uraia wa Tanzania na Wale waliochukua Urai wa Hapa , pamoja na watoto wao
waliozaliwa hapa ambao ni Wamarekani kwa kuzaliwa tunajisikia na tunaipenda
Tanzania kama wenzetu walioko Marangu au Kimanzichana. Tofauti iliyopo ni
kwamba sisi tuko huku na wenzetu wako Biharamulo. Watoto wetu wamezaliwa hapa
na Binamu zao wamezaliwa Chalinze. Sisi
sote na watoto wetu ni watanzania na tunataka tutambulike na kuwa na haki sawa.
Watanzania
wa Washington DC, tumekuwa tukishirikiana kwa hali na mali na Ubalozi wa Hapa kuitanganza nchi yetu na kuitetea na kuiletea
sifa nzuri Tanzania. Hivi Sasa Ubalozi wetu hapa Unaandaa sherehe za Miaka 50
ya Muungano na Ni sisi Watanzania wa Ughaibuni tutashiriki kwa Moyo Mmoja na
nguvu zote kuipeperusha bendera ya Tanzania kwa niaba ya nchi nzima.
Watato wetu wataonyesha utamu wa nyimbo ya Taifa la Tanzania . Viongozi wa Taifa
watazungumza na watanzania wa hapa na kujadili maendelea na muelekeo wanchi. Sisi
Ni Watanzania.
Iddi Sandaly,
Rais Wa Jumuiya Ya
Watanzania , Washington DC , Maryland
na Virginia.
3 comments:
The mdudu,ndugu zangu huko USA itabidi mtoke mtembelee nchi zote za ugaibuni ili tuwe pamoja zaidi hasa hasa nyie viongozi wa watanzania waishio ugaibuni so msiegamie sehemu moja tu ya WASHINGTON DC muwatembelee mabalozi wote wanaoiwakilisha Tanzania ili tupatekujijua idadi yetu hili swala lisichukuliwe kimasihara masihara lazima tuwe ngangali sote tunaipenda Tanzania yetu.
SEMA SEMA RAIS!
Hili suala hapa bongo halina mvuto kabisa. Hapa ni Mungano tu mpaka kieleweke.
Post a Comment