Samba Boys ruksa KUVUNJA AMRI YA 6
*Scolari awaruhusu Brazil kuwa na wapenzi wao
Kocha wa Timu ya Taifa ya Brazil, Luiz Felipe Scolari amewaruhusu
wachezaji wake kuendelea kuvunja amri ya 6 wakati wa mechi za Kombe la
Dunia linaloanza Juni mwaka huu nchini Brazil.
Scolari alisema kwamba hakuna marufuku yoyote ya wachezaji kuwa na
wapenzi au wake zao wakati wa mashindano hayo na kwamba watatakiwa
kuendelea na mfumo wao wa kawaida wa mapenzi na si vinginevyo.
Imekuwa kawaida baadhi ya timu kuweka marufuku ya wachezaji kuwa na wake
au wapenzi wao nyakati za mashindano makubwa kwa ajili ya kutaka
kuwaweka wachezaji kuwa katika mazingira ya kimchezo na kukita akili
kwenye mechi inayofuata.
England ni moja ya timu inayolaumiwa kwamba imekuwa ikifanya vibaya
kwenye michuano ya kimataifa kutokana na athari za kuwapo wake au
wapenzi wao kwenye kambi ya timu na kubadili maana nzima ya timu
ilichokwenda kufanya.
Samba Boys, hata hivyo, watakuwa huru kujirusha wakati wote wa mashindano lakini lazima wahakikishe wanakuwa fiti kimchezo wakati wote, ameonya kocha huyo maarufu aliyepata pia kuwafundisha Chelsea.
Samba Boys, hata hivyo, watakuwa huru kujirusha wakati wote wa mashindano lakini lazima wahakikishe wanakuwa fiti kimchezo wakati wote, ameonya kocha huyo maarufu aliyepata pia kuwafundisha Chelsea.
“Mapenzi kikawaida yanaruhusiwa kwa wachezaji wetu, kwa njia mbayo
itawapa uwiano mzuri na kwa mfumo usio mbaya maana kuna wengine
wanafanya mithili ya kuruka sarakasi, sasa hiyo haifai wala kuruhusiwa,”
akasema Big Phil ambaye pia ni Mbrazili.
Katika michuano ya Kombe la Dunia 2002 Scolari alikuwa mkali sana kwenye
masuala hayo, ambapo aliwapiga marufuku wachezaji wake kujiingiza kwa
namna yoyote ile kwenye vitendo vya ngono wakati wote wa mashindano
hayo, ili kuhakikisha wanatwaa kombe, na kweli wakalitwaa.
Ronaldo alikasirikia hatua ya kuzuiwa kufanya ngono, akasema pamoja na
kufurahia kutwaa kulinyanyua kombe hilo kwa furaha, kitu kingine ambacho
hatakisahau ni walivyozuiwa kufanya ngono na kocha huyo mkali hivyo
kumfanya awe na wakati mgumu kipindi chote cha mashindano hayo.
2 comments:
Kuvinja amri ya sita ni kufanya mapenzi na mtu ambaye siyo mke au mume wako. Sidhani kama kocha amewaambia wakalale na wanawake wasio wake zao kwa wale ambao wameoa.
That is the first symptom that Brazil won't WIN the World Cup!
Post a Comment