Adam Kuambiana enzi za uhai wake.
MWIGIZAJI na Muongozaji filamu maarufu Bongo, Adam Kuambiana amefariki dunia wakati akipelekwa hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam kwa matibabu alfajiri ya kuamkia leo. Marehemu alianguka chooni akiwa location katika hoteli ya Silver Rado iliyopo Sinza kwa Remy, Dar. Kabla ya mauti kumfika, Adam alikuwa akilalamika kuwa anasumbuliwa na tumbo. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!
Marehemu Kuambiana katika muonekano wake wa siku zake za mwisho za uhai wake
...katika pozi na msanii Irene Uwoya
...(kushoto) akiwa na wasanii wenzake JB (kutoka kulia), Tino na Mtangazaji wa Clouds TV, Zamaradi
Mwili wa Marehemu Adam Kuambiana ukitolewa nje ya Hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam kupelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuhifadhiwa leo mchana huu.
...Msanii aliekuwa akicheza filamu moja na marehemu katika Hoteli ya Silver Rado iliyopo Sinza kwa Remy, Dar akilia kwa uchungu nje ya Hospitali ya Mama Ngoma leo mchana huu.
Credit:GPL
No comments:
Post a Comment