ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 14, 2014

KINANA AVUTIWA NA MIPANGO YA KUSAIDIA VIJANA SIKONGE

  • Asema Vijana wa Pathfinders Green City ni mfano wa kuigwa.
  • Awataka wilaya zingine nchini kuiga mfano huo kwani utasaidia sana katika kuharakisha maendeleo kwa vijana,kuwajenga katika misingi bora ya mshikamano
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa taji la maua wakati wa mapokezi alipowasili kwenye Kata ya Pangale wilaya ya Sikonge mkoani Tabora ambapo anategemewa kufanya ziara ya siku 2 katika wilaya ya Sikonge.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akikaribishwa kwa wimbo maalum wa kizazi kipya na vijana wa Pathfinders Green City mara alipowasili kijijini hapo na kujionea miradi mbali mbali ya vijana ya kimaendeleo ambayo itasaidia sana kuwajenga vijana na kupuguza umasikini, katika kijiji hicho kuna vijana wa kiume 59 na wa kike 19.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akiwa amesimama karibu kabisa na mizinga ya nyuki, Mradi huu wa nyuki ni wa Vijana wa Pathfiders Green City ambapo wana mizinga 600 mpaka vihi sasa.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahan Kinana  akiwa mbele ya mizinga 600 ya nyuki kwenye mradi wa vijana wa Pathfinders  Gree City wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelekezo namna ya kufunga tumbaku ambayo imeshakaushwa na vijana wa Pathfinders Green City alipotembelea wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na vijana wa Pathfinders Green City nje ya chumba maalum cha kuhifadhia Tumbaku,wengine pichani ni Mkuu wa mkoa wa Tabora Fatma Mwassa  na Afisa kutoka TLTC Ndugu Goodluck Mmasi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali ya kisasa (hydraform bricks) kwenye mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa za makazi ya watu zinazojengwa na vijana wa Pathfinders Green City wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kubeba matofali kwenye mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa zinazojengwa na vijana wa Pathfinders Green City,Sikonge mkoani Tabora.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsaidia fundi kwa kumpatia matofali wakati wa ujenzi wa nyumba za kisasa zinazojengwa na vijana wa Pathfinders Green City,Sikonge mkoani Tabora.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Wilaya ya Sikonge Ndugu Bulele Jitala ambaye alimueleza Katibu Mkuu ujenzi wa nyumba kwa kutumia matofali ya hydraform ni wa gharama nafuu sana.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akichagua kandambili kwenye duka la kijiji cha Vijana cha Pathfinders Green City,Sikonge mkoani Tabora.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi vifaa vya ujenzi na ushonaji kwa George Sospeter Waimani  Mwenyekiti wa vijana wa Pathfinders Green City ambavyo vimetolewa na Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (Sido) mkoani Tabora.
  
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijaribu mkanda wa ngozi uliotengenezwa Tabora kwenye banda la maonyesho la Sido kulia kwake ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiangalia kiatu cha ngozi kilichotengenezwa kwa mkono.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na vijana wa Pathfinders Green City na kuwaambia amejifunza mengi kutoka kwao na amesema vijana hao ni mfano wa kuigwa katika kupunguza tatizo la ajira, kupunguza umasikini lakini pia kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuweka madirisha kwenye jengo la kituo cha afya cha Sikonge, mkoani Tabora.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akizungumza nje ya jengo linalojengwa kwenye kituocha afya cha Sikonge kushoto kwake ni Daktari Mfawidhi wa kituo hicho Dk. Fredrick Mtao.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na walimu wa Sekondari ya Kamagi mara baada ya kukagua ujenzi wa maabara, madarasa na nyumba za walimu katika shule hiyo hiyo iliyopo wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.

Moja ya Nyumba za Walimu wa shule ya Sekindari ya Kamagi,wilayani Sikonge mkoa wa Tabora.



No comments: