Kikosi cha Mbeya City
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Mwambusi alisema timu yake ilishiriki ligi kwa mara ya kwanza msimu uliopita na wachezaji wake wengi hawakua na uzoefu na mikikimikiki ya ligi lakini walijiatahidi na kumaliza katika nafasi ya tatu.
"Kama mambo yatenda kama nilivyopanga, msimu ujao tutafanya vizuri zaidi, wachezaji wangu tayari wameshaona ugumu wa ligi na changamoto zake hivyo msimu ujao watakuwa vizuri zaidi. Aidha, alisema asingependa kuuza mchezaji yoyote katika kikosi chake.
"Lakini soka la sasa hivi ni pesa, wachezaji wanaendesha maisha yao kwa kutegemea mpira hivyo wanaangalia zaidi maslahi," alisema Mwambusi, lakini "kama ni mipango yangu nisingependa kupoteza mchezaji hasa wale muhimu."
Kutokana na timu hiyo kufanya vizuri kwenye ligi, timu kubwa za Simba na Yanga zinawinda baadhi ya wachezaji wake nyota kwa ajili ya kuzichezea msimu ujao.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment