Thursday, May 15, 2014

Mtuhumiwa huyu wa wizi katika Mabenki anatafutwa

Kamishna Kova akionesha hadharani picha ya mtuhumiwa mbele ya wanahabari.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 


WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI JESHI LA POLISI TANZANIA


PRESS RELEASE


14/05/2014

POLISI WAMGUNDUA KINARA WA MTANDAO WA WIZI KATIKA MABENKI JIJINI D’SALAAM (PICHA YAKE YATOLEWA HADHARANI) ANATAFUTWA NA JESHI LA POLISI


Jeshi la Polisi Kanda Maalum D’Salaam limefanikiwa kumbaini mtuhumiwa mhimu ambaye ni kinara wa mtandao wa wizi katika mabenki ambaye anajulikana kwa jina laRONALD S/O MOLLEL umri miaka 37, mfanyabishara na mkazi wa Kimara BonyokwaJijini  D’salaam.

Mtuhumiwa huyu amekimbilia mafichoni mara baada ya tukio la ujambazi katika Tawi laBenki ya Barclays Kinondoni lililotokea tarehe 15/4/2014 ambapo majambaziwalifanikiwa kupora kiasi kikubwa cha fedha T.Shs.390,220,000/= , USD 55,000/= na EURO 2150/=. Aidha sasa imefahamika kwamba mtuhumiwa huyu ni mume wamtuhumiwa wa kwanza katika tukio la Barclays Benki aitwaye ALUNE D/O KASILILIKA @ ALUNE D/O MOLLEL , miaka 28, Mkazi wa Kimara Bonyokwa ambaye ni Menejawa Benki Tawi la Barclays Kinondoni. Mtuhumiwa Mollel anatafutwa kwa kila hali kwavile yeye ndiye alikuwa kinara wa kupanga tukio hilo la Barclays na mara baada ya tukioametoroka na kiasi kikubwa cha fedha hizo zilizoibiwa.

Zipo taarifa za kuaminika kuwa mtuhumiwa huyu amekuwa akipanga na kushirikikikamilifu katika matukio mbali mbali ya uhalifu mkubwa ikiwa ni pamoja na kuongozavikundi vya majambazi vilivyowahi kupora katika mabenki mbali mbali katika kipindi chamwaka mmoja uliopita. Mtuhumiwa huyo ni hatari kwani ana mtandao na watumishimuhimu katika matawi mbali mbali ya mabenki kwa lengo la kufanikisha uhalifu katikamabenki hayo.Jeshi la Polisi limelazimika kutoa picha yake hadharani kwa kutumia dhana ya ulinzishirikishi ili mtuhumiwa huyu akionekana akamatwe na taarifa zitolewe katika kituo chochote cha Polisi ikiwa ni lengo la polisi kupambana na uhalifu katika dhamira yakuzuia uhalifu, kulinda maisha na mali za wananchi. Zawadi nono ya fedha taslimitatolewa kwa siri kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwamtuhumiwa huyu. Pamoja na maelezo hayo mtuhumiwa mwenyewe sasa anapewafulsa ya kujisalimisha katika kituo chochote cha polisi kabla ya kukamatwa kwa njianyingine.
RONALD S/O MOLLEL, mtuhumiwa wa ujambazi katika mabenki mbalimbali jijini Dar es sSlaam, anayetafutwa na Polisi.

No comments: