ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 14, 2014

PITA PITA YA VIJIMAMBO WASHINGTON DC

Timu ya T.E.S ndani ya jiji la watunga sheria hapa ni, Dr Temba Engineer wa T.E.S akinyoosha maelezo kwa wasaidizi wake jinsi ya kuifanya kazi yake kwa ufasaha. T.E.S Company yenye makao makuu yake Brooklyn. NY, wamepiga kambi Washington DC kikazi zaidi kwa muda wa wiki mzima kujenga banda na kufunga mashine ya kukaushia samaki. (Smoke House) katika kiwanda kilichopo 1900 Fenwick St NE. Washington. DC.
Hapa hadi kieleweke Dr Temba akitoa maelezo ya nini cha kufanya. Huyu jamaa  kushoto kwa Dr Temba kazi aliyosomea ni upishi, ilikuwa siyo kazi rahisi kufanyanae kazi mtu aliezowea vitunguu na nyanya na ukaingilia kazi nyingine nje ya ulichokisomea si mchezo. Na upande wa kulia kwa Dr Temba jamaa kazi yake ni ya ujenzi wa kutumia matofali na hapa ni kuunganisha vyuma kwa moto. Lakini kazi ilienda vizuri na kutoa sura ya maendeleo.


No comments: