ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, June 18, 2014

ALIYESHAMBULIA UBALOZI WA MAREKANI BENGHAZI, AKAMATWA

Rais wa Marekani Barrack Obama anasema mshukiwa mkuu wa mashambulizi yaliyotokea katika Ubalozi wa taifa hilo mjini Bengazi nchini Libya na kusababisha Balozi wa Marekani nchini humo mwaka 2012 amekamatwa.
Obama amesema, mshukiwa huyo
Ahmed Abu Khattala (PICHANI) alitiwa mbaroni na kikosi maalum cha Marekani na tayari ameanza kusafirishwa kwenda Marekani kujibu tuhuma zinazomkabili, amethibitisha waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry.
Msemaji wa shirika la ujasusi nchini Marekani John Kirby amemtaja Ahmed Abu Khattala kuwa gaidi nambari moja kaongeza kuwa Khattala ni miongoni mwa walioratibu mashambulizi kadhaa dhidi ya majengo yanayomilikiwa na Marekani huko Lybia.
Wakati wa mashambulizi hayo Balozi wa Marekani Chris Stevens na watu wengine watatu walipoteza maisha.

No comments: