Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Henry Kapufi wakisikiliza maelekezo juu ya ufugaji nyuki kutoka kwa mmoja wa wafugaji(hayupo pichani) katika kijiji cha mabilioni wilayani Same katika siku ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame duniani.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu akipanda mti wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa duniani zilizofanyika katika kijiji cha mabilioni wiayani Same.
Sehemu ya umati wa Wananchi waliojitokeza katika kuadhimisha siku ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame duniani iliyofanyika kitaifa katika kijiji cha mabilioni wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro.
Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu akiongea na wananchi katika maadhimisho hayo .
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu akicheza ngoma ya msanja sanjari na kikundi cha wakinamama wa kijiji cha mabilioni wilayani Same katika maadhimisho ya siku ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame duniani.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu akihutubia katika siku ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame duniani. Kitaifa maadhimisho ya siku hiyo yamefanyika katika kijiji cha mabilioni Tarafa ya Hedaru wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro.
Wito
umetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwaimu kwa jamii ya Umma wa Tanzania kutunza
ardhi na udongo kwa ajili ya matumizi endelevu na kuifanya ardhi iwe na uwezo
wa kuzalisha mazao ya kilimo na mifugo na kutoa huduma zingine muhimu ili
kuepuka hali ya jangwa na ukame kwa kizazi cha sasa na kijacho na pia kuchukua
hatua madhubuti za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mheshimiwa
Mwalimu amesema hayo wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya kupambana na
kuenea kwa hali ya jangwa na ukame duniani. Maadhimisho hayo kitaifa
yamefanyika katika kijiji cha Mabilioni tarafa ya Hedaru wilayani Same mkoa wa
Kilimanjaro.
Aliongeza
kuwa takwimu zinaonyesha kuwa robo ya dunia ambayo ni zaidi ya hekta bilioni
3.6 inatishiwa na janga la kuenea kwa hali ya ukame na jangwa. Hivyo basi
alisema ni wajibu wa kila mmoja kulinda
ardhi ili iweze kuleta manufaa baadaye sababu kuenea kwa hali ya jangwa na
ukame kunasababisha matatizo ya kiuchumi,kimazingira na kijamii . Vivyo hivyo
kuenea kwa hali ya jangwa na ukame kunapelekea ardhi kupunguza uwezo wa
kuzalisha mazao ya chakula na kuongeza umaskini .
Mwisho
alitoa wito kwa Hamashauri zote Nchini kuunda kamati za Mazingira kuanzia ngazi
ya kijiji mpaka Wilaya. Pia aliomba vyombo vya habari Nchini kuendelea kutoa
elimu na kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kuchukua njia thabiti za kupambana
na kuzuia kuenea kwa hali ya jangwa na ukame.Kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa ni
Ardhi ni mustakabali wa maisha, tuilinde
dhidi ya uharibifu.
No comments:
Post a Comment