NGOMA AFRICA BAND AKA FFU UGHAIBUNI WAWATIA WAZIMU WASHABIKI !
INTERNATIONA AFRICAN FESTIVAL TUBINGEN 2014 PALIKUWA HAPATOSHI !
Nyuma ya Polisi !Jukwaani FFU ! ,Mbele ya Jukwaa washabiki waliodata akili !
Tubingen,Ujerumani,Ilikuwa usiku jumamosi 19.Julai 2014 bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni " imefanikiwa tena kuwatia wazimu malefu ya washabiki katika maonyesho makubwa ya International African Festival 2014 mjini Tubingen,Ujerumani.
Bendi hiyo iliyobatizwa majina mengi ya utani na washabiki wake imejukuta inaongeza idadi ya maelfu ya washabiki katika maonyesho yake.
Katika hali isiyo ya kawaida usiku wa jumamosi 19.Julai 2014 Ngoma Africa band
imejikuta ipo ikitingisha jukwaa kwa muziki moto moto ambao mbele ya jukwaa kulikuwa na umati wa washabiki na nyuma ya jukwaa kukiwa na magari maalumu ya Polisi wa kuziwia ghasia wa kujerumani ambao walikuwa tayari kwa lolote lile!
Maelfu ya washabiki wakiwa wanajirusha bila ya mashaka na muziki wa FFU-ughaibuni aka viumbe wa ajabu Anunnaki Alien ukipenda watoto mbwa chini ya uongozi wake mwanamuziki Ebrahim Makunja aka kamanda Ras Makunja.
Wadau mbali mbali walihojiwa katika maonyesho hayo wameitaja bendi hiyo kila
kukicha inazidi kujizolea wingi la umati wa washabiki kutoka na mvuto na umahili wake. Ngoma Africa band inatajwa ndio bendi pekee ughaibuni inayoongoza kuwa na washabiki wa lika,jinsia na mataifa mbali mbali.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi
No comments:
Post a Comment