NAAMINI UMECHEZA SOKA ENZI UKIWA MDOGO, HIZI NDIYO SHERIA TULIKUWA TUNAZITUMIA NA IKIWEZEKANA KILA MKOA, WILAYA NA KITONGOJI ZILIFANANA KABISA!
1. dogo mnene lazima awe
Golikipa
2. Mwenye mpira ataamua nani
acheze na nani asicheze.
3. Penalti itatokea tu pale
mchezaji akiumia sana na kutoka
damu.
4. Mechi itaisha kama kila
mchezaji atakua amechoka.
5. Hakuna free kick, kitu kama icho
hakipo kwenye mechi zetu, labda mbabe mmoja alazimishe na anaweza kuweka sehemu anayotaka yeye bila ya kujali madhambi yametokea eneo gani, huenda kwa kuwa hakuna spray kama vile World Cup Brazil.
6. Hakuna refa, mchezaji anaweza
kuzunguka na mpira ata nyuma ya
goli.
7. Kama haushiriki kwenye
kutengeneza mpira unaweza
usipate namba uwanjani.
8. Ukichaguliwa mwishoni ujue
uwezo wako ni mdogo kuliko watu
wote uwanjani.
9. Wale ambao wamekosa namba
kazi yao ni kufata mpira ukitoka,
au kutungua mpira endapo
utanasa kwenye mti uku
wakisubiria mchezaji aitwe kwao
na wao wapate nafasi.
10. Mwenye mpira akikasirika,
mechi ndo itakua imefika mwisho.
11. Inaruhusiwa kubadili golikipa
kama penalti ikitokea na baada ya
penati golikipa anaweza
kuendelea yule wa mwanzo.
12. yule mtaalam wa soka huwa
hakosi namba ata siku moja.
13. Mwenye mpira huwa hatolewi
ata akicheza vibaya.CREDIT:SALEH JEMBE
warm up, TOBO BAO
ReplyDeletemwenzako akikupiga tobo anaruhusiwa kukupiga kibao sehemu yeyote ya mwili. hahahhah