Thursday, July 3, 2014

Tahadhari ya mashambulizi Uganda


Polisi wako macho mjini Kampala
Polisi nchini Uganda wamedhibiti usalama mjini Kampala kufuatia onyo la mashambulizi ya kigaidi kupangwa kufanywa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebe.
Maafisa wa usalama katika
uwanja huo, walisema kuwa onyo la shambulizi hilo lililopangwa kufanyika Alhamisi linapaswa kuchukuliwa kwa uzito.
Marekani ilitoa tahadhari na kuwashauri raia wake waliokuwa na nia ya kusafiri kwenda nchini humo Alhamisi kubadili mipango yao.
Kundi la wanamgambo la Al shabaab lilishambulia mikahawa miwili mjini Kampala mwaka 2010 wakati wa fainali ya kombe la dunia nchini Afrika Kusini.
Zaidi ya watu 70 waliuawa katika mashambulizi hayo, wakati ambapo washambuliaji wa kujitoa manga walipojilipua wakati mashabiki wa soka walikuwa wakitazama michuano hiyo.
"kulingana na taarifa za ujasusi, kuna tisho maalum dhidi ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebe na kundi la kigaidi lisilojulikana. Tisho hilo haliwezi kuchukuliwa kwa wepesi, '' ilisema taarifa ya maafisa wa usalama.
Taarifa hiyo ilisema kuwa shambulizi lilipangwa kufanywa kati ya saa kumi na mbili jioni na saa mbili usiku.
Vikosi vya usalama vimeweka vizuizi katika uwanja huo na katika baadhi ya barabara zilizo umbali wa kilomita 32 kutoka uwanja huo.
Mikutano kadhaa ya kimataifa inafanyika nchini humo na lengo la maafisa wa usalama ilikuw akuwahakikishia usalama wao wajumbe wanaohudhuria mikutano hiyo.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake