By Israel Saria on July 21, 2014
Timu ya Tanzania inayoshiriki michezo ya Jumuia ya Madola Glasgow 2014 leo alasiri impokelewa rasmi katika kijiji cha michezo hapa Glasgow Scotland.
Katika sherehe hiyo fupi ilioandamwa na kupandishwa kwa bendera na kupigwa wimbo wa taifa ulijumuisha wanamichezo40 ikiwemo pamoja na viongozi.
Sherehe hizo zilizofana sana pia zilihudhuriwa na Afisa ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza Ndugu Amos Msanjila.
Wakati huo huo Naibu waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Ndugu Juma Nkamia kesho asubuhi anatarajia kutembelea wanamichezo wa Tanzania hapa kijiji cha michezo.
Pamoja na Naibu waziri wengine wanao taraji kufuatana naye ni Rais wa Kamati ya Olimpiki nchini Ndugu Gulam Abdallah na Katibu mkuu wa TOC ndugu Filbert Bayi.
Michezo inataraji kufunguliwa rasmi siku ya Jumatano na Malkia wa Uingereza katika sherehe zinazotarajiwa kuanza saa tatu usiku.
TANZANIA SPORTS
No comments:
Post a Comment