ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 5, 2014

MAJI YA UPONYAJI YAUA WATOTO WAWILI, MTUME NA MAMA WA WATOTO WASHIKILIWA NA POLISI


Mtume Austin Eduviere anayeuza maji hayo ya uponyaji.
Watoto wawili wa familia moja nchini Nigeria Wisdom Clement (2) pamoja na mdogo wake Prayer Clement mwenye miezi 9 wamefariki dunia baada ya mama yao kuwanywesha maji ya baraka aliyonunua kutoka kwa mmoja wa wachungaji kwa ajili ya uponyaji.

Mama huyo aitwaye Ese Oghenevwe 25 pamoja na mchungaji aliyetoa maji hayo Austin Eduviere wa kanisa la Triumphant World International lililopo Abraka wamekamatwa na jeshi la polisi kutokana na vifo vya watoto hao kama ilivoripotiwa na mtandao wa Vanguard. Kwa mujibu wa kituo cha polisi Abraka wamesema walipata ripoti majira ya saa kumi za alfajili tarehe 25 Julai kwamba Oghenevwe amewaua watoto wake kwa kuwapa maji ya kunywa.
Kutokana na taarifa tulizopata, ofisa upelelezi alimkamata Ese Oghenevwe. Uchunguzi umebaini kwamba maji hayo alipewa na mmoja wa mitume kwa ajili ya uponyaji huku mtume naye akitabainisha kwamba aliyaombea maji hayo" imeeleza taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi. Aidha taarifa hiyo imeeleza kwamba mtume Eduviere amekamatwa akilisaidia jeshi la polisi katika uchunguzi wao. Uchunguzi unasema maji hayo yalikuwa yamechangwa na chumvi na kuyauza kwa watu kwa kiasi cha Naira za Kinigeria 1,850 sawa na shilingi 19,071 akidai huponya magonjwa mbalimbali baada ya kuyaombea, taarifa hiyo imesema.

Muuguzi aitwaye Susan Gidiagba ambaye ni nesi anayetambuliwa na kufanya kazi katika hospitali ya Baptist ya Eku nchini humo, kupitia ukurasa wake wa facebook aliandika kwamba msichana mmoja alijifungia ndani ya chumba cha watoto wake akiwapa maji ya upako bandia kama alivyosema na mumewe alipovunja mlango kuingia ndani alikuwa tayari amechelewa.

"Nilikwenda kushuhudia kwa macho yangu kituo cha polisi tukio hili lilipotokea…. mumewe pia amesema mkewe alikwenda chumbani kwa watoto wao na kujifungia kufanya kitendo hicho…. mlango ulivunjwa na mumewe baada ya mwanamke huyo kukataa kutoka na akishuhudia akiwaingiza vidole mdomoni watoto ….. na kudai kwamba yalikuwa mafuta ya upako aliyopewa na mchungaji kuyatumia kwa watoto wao kwasababu walikuwa wagonjwa… maajabu hayaishi….Mungu tulinde watoto wako mikononi mwa wabaya" aliandika Gidiagba kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Wanaigeria wengine wakaenda mbele zaidi na kuuliza "inakuwaje mtumishi wa Mungu kuuza maji ya uponyaji kama yanatoka kwa Mungu? kwasababu Yesu aliwaambia wanafunzi wake 'Mmepewa bure toeni bure'. Mpaka tusafishe mioyo yetu na kupokea neno lake likae ndani na mpaka macho yetu yafunguke, vinginevyo shetani na wachungaji wake wa uongo ama bandia wataendelea kushikilia akili za watu" alisema Akintayo Olanusi katika facebook.

"Kwakupigwa kwake tumeponaa nasio kwakunywa kitu chochote kilichonunuliwa kwa mchungaji. Hii ni biashara tu" aliandika Oluwatuyi Alasoadura.

No comments: