ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 6, 2014

MKUU WA MKOA WA MTWARA ATEMBELEA BANDA LA JESHI LA MAGEREZA MAONESHO YA NANE NANE KITAIFA, MKOANI LINDI

 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia(kushoto) akiwasili katika Banda la Jeshi la Magereza tayari kujionea shughuli mbalimbali zenye tija zinazofanywa na Jeshi la Magereza(kulia) ni Mkuu wa Banda la Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mlasani Kimaro akimuongoza Mkuu wa Mkoa wa Mtwara katika sehemu mbalimbali za Banda la Jeshi la Magereza alipotembelea leo Agosti 4, 2014 katika Viwanja vya Maonesho ya Nane Nane Kitaifa, Mkoani Lindi.
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia(aliyevaa Kombati) akiangalia mazao ya chakula yanayolimwa  katika Magereza mbalimbali hapa nchini kama yanavyoonekana katika picha. Jeshi la Magereza katika kutekeleza jukumu lake la kuwalinda na kuwarekebisha Wafungwa huwapatia pia mbinu na Stadi za Kilimo bora ili waweze kuzitumia wanapomaliza vifungo vyao huko katika jamii zao.
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia akifurahia ubora wa bidhaa za ngozi zinazozalishwa na Jeshi la Magereza katika Kiwanda chake cha Viatu cha Gereza Karanga Moshi, Mkoani Kilimanjaro(kushoto) ni Afisa Masoko wa Shirika la Magereza, Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Yunge Saganda akionesha kiatu cha ngozi aina ya travota(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Banda la Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mlasani Kimaro.
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Mstaafu Simbakalia akitembelea Mabanda ya Mifugo ya Jeshi la Magereza mara tu baada ya kuwasili katika Banda la Jeshi la Magereza(kushoto t-sheti ya blu) ni Mtaalam wa Mkfugo(ndege) Sajini Taji Nesia Hozza toka Gereza la Wanawake, Kingolwira Mkoani Morogoro akitoa ufafanuzi wa Kitaalam namna Ufugaji wa kuku unavyopaswa kufanyika.
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia(aliyevaa Kombati) akipata elimu ya Shamba Darasa toka kwa Mtaalam wa Kilimo cha Mbogamboga wa Jeshi la Magereza, Sajini Taji Oliva William(mbele t-sheti ya blu) toka Gereza Nachingwea namna Bustani za Mbogamboga zinavyostawishwa kwa kuzingatia Kanuni za Kilimo cha Kisasa na Biashara(wa Nne kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Lindi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Tusekile Mwaisabila.
Mkuu wa Banda la Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mlasani Kimaro(wa kwanza kulia) akikabidhi zawadi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia(aliyevaa Kombati) alipotembelea Banda hilo leo Agosti 04, 2014 katika Viwanja vya Maonesho ya Nane Nane vya Ngongo, Mkoani Lindi. Kanali Mstaafu Simbakalia amelipongeza Jeshi la Magereza kutokana na ubunifu mkubwa uliopo katika shughuli zake mbalimbali zilizopo katika Banda hilo(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

No comments: